DC Akanusha Taarifa Zinazoenezwa Kuhusu Viongozi Wa Chadema


Mkuu wa wilaya ya Miraji Mtaturu Ikungi amekanusha taarifa za kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa wakiratibu michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu na badala yake aliwaweka ndani kwa sababu walitaka kuandamana bila kibali.

Kupitia taarifa aliyoitoa Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii zina lengo la kwafitinisha wana Ikungi na jimbo la Singida Mashariki kwa ujumla.

Amesema kuwa "Viongozi waliokamatwa na baadaye kuachiliwa walihojiwa na kuachiwa kwa dhamana hawakuwa wakiratibu michango bali walikuwa wakiandika mabango yenye ujumbe wa kichochezi dhidi ya viongozi wa serikali na wakitaka kuandamana bila kibali.

Aidha amewataka wanaikungi kutulia katika kipindi hiki ambacho Mh. Lissu akipatiwa matibabu nje ya nchi na pia kutojaribu kuingiza siasa na badala yake waiachie serikali nafasi ya kuendelea na kazi ya uchunguzi ili waliohusika na tukio hilo waweze kuchukuliwa hatua kali.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa "Ingawa viongozi wa CHADEMA Taifa wameshatangaza utaratibu wa kuchangia, ningewashauri na viongozi wengine wafuate mkondo huo huo. Mimi kama kiongozi wa wilaya tayari nimeshamwagiza mwenyekiti wa Halmashauri ya Ikungi ili kuitisha kikao cha madiwani ili kuweka utaratibu wa pamoja wa namna ya kuchangia matibabu ya mbunge wetu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad