Diamond Platnumz inabidi Apewe Uwaziri au Ukuu wa Mkoa Kwa Maana Amelifanyia Mambo Makubwa Sana Taifa Hili

Diamond Platnumz inabidi Apewe Uwaziri au Ukuu wa Mkoa Kwa Maana Amelifanyia Mambo Makubwa Sana Taifa Hili
Huyu bwana mdogo Diamond Platunumz amefanya mambo mengi makubwa makubwa sana hapa nchini kuliko hata viongozi wemye dhamana hiyo tena amemzidi hata rais magufuli kwa kujitolea misaada mbalimbali kwa wananchi wenye uhitaji.

Kwa haraka haraka ukipiga mahesabu misaada aliyoitoa kwa miaka kadhaa inafikia Bilioni 20+.

Asilimia kubwa ya mapato yake hutumia kusaidia vijana na wazee wasiojiweza.


Wasanii chipukizi wengi wamepewa sapoti ya kimawazo na kifedha na diamond platnumz ingawaje wakishatoka wanasahau fadhila .

 Hawa watoto wamepata bahati ya kusomeshwa shule ya kimataifa inayofanya mtaala wa Cambridge na ada isiyopungua milioni 20 kwa mwaka mpaka watakapo fika ngazi ya chuo kwa kitendo chao tu cha kuibuka washindi kwa kucheza ngololo.


Mbali na haya diamond pia amechimba visima vya maji visivyopungua 15 kwa shule mbalimbali hapa nchini hususani kwa mkoa wa dar es salaam.

Katika kusaidia vijana diamond pia hayupo nyuma ,kuna wakati alikuwa anamlipa Haruna Moshi Boban nusu ya mshahara anaolipwa kipindi anachezea timu ya Friends Rangers.

Vilevile amesaidia kwa kiasi kikubwa sana kukuza na kuibua vipaji vya wasanii mbalimbali hapa nchini kwa mfano Rayvan kipindi yupo Tip Top alikuwa hajulikani sana na ila Mondi akamchukua na kumsaidia kumtangaza mpaka akafanikiwa kuchukua tuzo ya BET mwaka huu ,wasanii wengine kama vile Harmonize ,Lavalava queen darlin nk.


Pia diamond hayupo nyuma kusaidia wasanii wenzake , mara kwa mara amekuwa akiwasaidia kuwapa pesa za kufanyia video wasanii wenzake na vilevile huwapa ofa ya kuchagua mavazi kwenye maduka yake ya nguo mara kwa mara.

Diamond pia alimsaidia Diva kumnunulia simu yenye thamani isiyopungua milioni moja.


Pia hata zile milioni 13 alizotoa Wema kumdhamini kajala zilitoka mikononi mwa diamond ila hakutaka ijulikane kwa watu wengi.


Diamond mara kwa mara amekuwa akisifika kuwanunulia magari wasanii wenzake hasa katika sherehe za siku zao za kuzaliwa.

Diamond vilevile hayupo nyuma kwenye kusaidia mambo ya dini kuna kipindi alitaka kujenga msikiti utakao kuwa mkubwa kushinda yote hapa Africa Mashariki ingawaje suala hilo lilipingwa vikali sana na viongozi wa dini kwa kudai kuwa pesa zake ni haramu hazifai kujengea msikiti na hata kama akijenga yeye diamond hatopata thawabu zozote kwa hiyo itakuwa sawa na bure tu .


Diamond mara kwa mara amekuwa akisaidia wakina mama wasiojiweza kwa kuwapa misingi ya biashara ili kuweza kuendesha maisha yao.

Diamond pia amekuwa akiwapa motisha walimu kutoka shule mbalimbali anazozitembelea kwa kuwapa pesa na nyenzo za elimu za elimu kama vile vitabu nk.

By Hance Mtanashati


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama kungekuwa na nafasi ya waziri wa ngono na uchepukaji katika baraza la mawaziri basi labda Diamond wako angekuwa na madai ya kufikiriwa nyazifa fulani katika serikali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad