Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amelamba shavu nono la kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya vinywaji vikali ya Luc Belaire ya nchini Ufaransa.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kampuni hiyo imethibitisha kuwa Diamond Platnumz atakuwa mwanafamilia mpya kwenye kuitangaza bidhaa hiyo na kuungana na Mastaa kibao duniani ambao pia ni mabalozi wa bidhaa hiyo akiwemo Rick Ross.
Baada ya taarifa hizo rapa kutoka Marekani Rick Ross, nae pia alimkaribisha Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika ‘Self Made Tastes Better’ caption iliyoambana na picha ya Diamond Platnumz .
Dili hilo ambalo bado halijawekwa wazi ni kiasi gani Diamond Platnumz ataingiza baada ya kusaini na kampuni hiyo, lakini huenda likawa ni dili la mamilioni ya fedha kwani Rick Ross ambaye pia ni Balozi wa Belaire anakadiriwa kulipwa kiasi cha Dola milioni 4.1, zaidi ya Tsh bilioni 8.
asisahu na kuiba views kwenye u tube. aonekane nyimbo zake ziko juu.
ReplyDeletekwahiyo tufanyeje kama kapata dili, si aendelee kuzaa halafu awakatae watoto.
ReplyDeletejamani na ile ndoa tulotangaziwa na pete ya dola 9. iliishia wapi? sasa baba Abdulnaseeb kapata dili lenye pesa nyingi, so Ajuza si atanenepa kwa kuvaa Almasi feki.
ReplyDeletekweli wewe ni kijana wa kiislamu i dought mhh jamani mujitambue sio mnafata ya dunia utaviacha na je umejtayarisha na ya kesho rudi kwa mola wako mbn unavuka mpaka lakini hata unakunywa pombe so you can d anything ila nakupa ushauri achana na vitu vya kuvuka mipaka ya dini yako
ReplyDeletekweli wewe ni kijana wa kiislamu i dought mhh jamani mujitambue sio mnafata ya dunia utaviacha na je umejtayarisha na ya kesho rudi kwa mola wako mbn unavuka mpaka lakini hata unakunywa pombe so you can d anything ila nakupa ushauri achana na vitu vya kuvuka mipaka ya dini yako
ReplyDeletehhe hhe vichekesho ukikosa hili unatafita lingine haya kubwa lipi hata hamorapa anapata hayo madili makubwa umeishiwa wakati umepita mpe raha ajuza wako nae ni pakacha
ReplyDeleteKuimba si vibaya. Yeye kama msanii anaweza. Asidharau tu au kukebei. Akumbuke pia umaarufu una mwisho. Kosa kila kitu uwe na Utu, usiwafanye watoto kama mziki wako. watoto ni Maisha, kama unaakili kweli, jiheshimu kwa kutowaingiza watoto wasiona hatia kwa kuwadharilisha. Kuna malaya wengi barabarani lakini watoto wao wanalingwa nyumbani. Kwa hili tu najua hujiheshimu. pesa, nyumba, magari, wanawake vyote hivi vimekuacha uchi kabisa. Watu wamekuona mpaka ndani. Hata chupi haiwezi kukusitiri. Mzee yupo nje na mkononi masaa ishirini na nne tayari kucchomeka.Ni ugonjwa unaohitaji tiba.Sijui hadhi ya wazee wako ikoje.Siwaelewi sawasawa.
ReplyDelete