Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop kutoka Mwanza, Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, amesema anasikitishwa na hatama ya maisha ya kizazi cha sasa, kwani kimeharibiwa kwa kiasi kikubwa na mitandao.
Rapa huyo amesema kizazi cha sasa hakina muda kabisa wa kujisomea vitabu ili waweze kujiongezea ujuzi, kwani mabadiliko ya teknolojia yamechukua sehemu kubwa ya maisha yao.
“Nawaonea huruma sana watoto wa kizazi hichi, mtu anatoka mapumziko anakutana na stori ya Alikiba katoa fresh remix, itamvuruga kabisa kwenda kuzingatia somo la hesabu ambalo linafuatia, sijui tunafanyaje lakini nawaonea huruma sana, sababu mi ni zao la analojia”, Fid Q alikiambia kipindi cha Bongo Fleva Top 20 cha EA Radio weekend hii.
Fid Q ambaye kwa sasa yupo na kazi mbili sokoni ambazo ni ‘Ulimi Mbili’ na ‘Fresh’, amesema kwa kipindi hiki cha digitali anapata changamoto kubwa anaposoma vitabu mitandaoni, kwani muda mwengine hukutana na matukio mengine yanayomfanya asitishe zoezi hilo, tofauti na kama angekuwa anasoma kitabu cha kawaida.
kajembe mbeleee. hatoi mtu kiki.
ReplyDelete