Msanii wa filamu bongo, Duma amedai kwamba muigizaji mwenzake, Gabo Zigamba ndiye chanzo cha sanaa ya filamu kulega kwani ameaminiwa na watanzania wengi lakini ameshindwa kuwatendea haki kwa kutoa kazi tangu alipopata tuzo mwezi wa 12 mwaka jana.
Povu la Duma limekuja hivi karibuni alipofanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari kumpelekea kusema kuwa Gabo ni kirusi kwenye filamu za bongo kwani anashindwa kujituma kama jinsi yeye anavyofanya
"Soko la filamu nchini ukweli halipo vizuri hususani kulega kwa filamu. Lakini yote haya yanasababishwa na Gabo kwa kushindwa kufanya kazi zake kama msanii. Unajua Watanzania wanamapenzi makubwa na Gabo lakini yeye ni msanii asiyejali. Alipopata tuzo mwaka jana tulijua kuwa angefanya mambo makubwa lakini cha ajabu ndiyo mzimekwenda kumpoteza. Naona anafurahi kuziona zikiwa zimejaa vumbi huku wananchi wakilia kupata muvi" Duma.
Duma ameongeza kuwa "Kuwapa watu filamu za 'online' hakukati kiu ya watu kutaka kuona kitu unachokifanya. Mfano mimi hapa nina muvi zangu nyingi zilizopo sokoni na zinafanya vizuri sana. Je yeye kwa nini asiitwe virus kwa kushindwa kufanya kazi? Sanaa inamuhitaji lakini yeye haijali ndiyo maana haoni umuhimu wa kufanya hata kazi za kimataifa.
Pamoja na hayo Duma amesema Gabo hana hadhi ya kuitwa staa kwani hana muonekano wa kisanii ndiyo maana anakosa hata mialiko mikubwa mikubwa.
"Gabo hana ustaa wowote, hana muonekano wa kisanii. Msanii gani anavaa suti moja kwenye 'event' tatu tofauti. Kama wewe ni msanii unatakiwa uwe na Swagg, muonekano uwe mzuri uweze kupata mialiko hata ya special appearance kwa sababu hajui atatokaje. Duma aliongeza.
"Mimi nafanya kazi, Gabo ni kirusi kwenye tasnia ya filamu. Kwahiyo kama anataka kubadilika abadilike kwasababu huwezi kuwa staa halafu unaishi maisha sawa na watu wa kawaida. Mimi siyo shabiki wake na wala yeye siyo role model wangu lakini namwambia atoe kazi" alimaliza
Hata hivyo Baada ya Gabo kupigiwa simu kuhusu kujibu tuhuma za Duma alisema hawezi kumjibu Duma anaye mtuhumu hajui kuigiza, kwani mwaka 2017 watu sio wajinga tena.