Mrisho Gambo amesema kuwa katika maisha ya kawaida siku ambayo mtu akifukuzwa kazi ndipo anaweza kugundua kuwa anaweza kuishi maisha yake vizuri bila ya kuwa na hiyo kazi na siku ambayo vijana wengine wanaweza kuanza kutumia vipaji vyao watagundua kuwa wanaweza kuishi bila kutegemea vyeti vyao.
"Siku utakayofukuzwa kazi utashangaa kuwa unaweza kuishi bila hiyo kazi, siku utakayoanza kutumia kipaji chako utashangaa kuwa unaweza ishi bila Digrii yako, siku Utakayoanza kutumia Ubunifu au Kutumia Taaluma yako utagundua kuwa unaweza kuishi bila kutegemea kupandishwa cheo, mengi unayodhani huyawezi ni kwa sababu tu una njia mbadala" alisema Mrisho Gambo