Hakimu Hawa Mbogo Achukizwa na Upande wa Jamhuri Kushindwa Kumpeleka Sethi Hospitali kwa Matibabu

Hakimu Hawa Mbogo Achukizwa na Upande wa Jamhuri Kushindwa Kumpeleka Sethi Hospitali kwa Matibabu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imechukizwa na upande wa mashtaka kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumpeleka mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme IPTL, Harbinder Sigh Sethi akatibiwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Sethi, Melchisedeck Lutema kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Sethi hajapelekwa Hospital ya Muhimbili kama Mahakama ilivyoagiza.

Lutema alidai kuwa katika mashauri yaliyopita Mahakama ilitoa amri mara kadhaa ikielekeza mshitakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.

”Naiomba Mahakama itumie busara ili kuhakikisha mshtakiwa anapelekwa Hospital na kwamba wa kuthibitisha kama ametibiwa au la ni mshtakiwa mwenyewe.”

Hakimu Shaidi alipomuuliza Sethi kama ameshatibiwa, alijibu hajatibiwa na kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi alisisitiza mshitakiwa huyo apelekwe katika Hospitali ya Muhimbili kama ilivyotoa maagizo awali.

”Ni wazi oda ya Mahakama lazima ifuatwe, haiwezekani kila siku tukija hapa tunaongea kitu kimoja tu hii haipendezi.”

Alisema mshtakiwa anatakiwa kupelekwa Muhimbili kwa sababu maalumu walizoeleza hapo awali kuwa ana puto tumboni.

”Nia ya kufanya hivyo ni afya ya mshtakiwa ili awe na afya njema. Hakuna sababu za kuja Mahakamani kama amri za Mahakama zinakuwa hazifuatwi. Naendelea kusisitiza na haifurahishi naomba apelekwe Hospitali.”

Awali katika kesi hiyo Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai alidai  shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kudai kuwa mshtakiwa alipelekwa Hospitali ya Magereza na kwamba alitibiwa na mtaalamu Dotto Pakacha ambaye anampatia matibabu kila anapolalamika huwa wanamuona.

”Kwa utaratibu wa Hospitali, Magereza hawajawahi kuwasilishiwa vyeti vya matibabu ili Daktari ajue anaanzia wapi kwenye kutoa matibabu.”

Aidha, alidai mshtakiwa alishapelekwa Hospitali ya Amana na kutibiwa na jopo la madaktari ambao walichukua vipimo ili wakamfanyie MRI Muhimbili.

”Tunaendelea na upelelezi kwa sababu kuna mashtaka ya kughushi yanahusisha Taasisi zaidi ya moja. Tunaomba Mahakama itupe muda ili tukamilishe upelelezi.”

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi September 29, 2017.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad