Hali ya Ukavu Katika Baadhi ya Maeneo Yaja- TMA

Hali ya Ukavu Katika Baadhi ya Maeneo Yaja- TMA
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imesema mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha msimu wa mvua wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema hayo leo Jumatatu mikoa itakayoathirika ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro na visiwa vya Unguja na Pemba.

Dk Kijazi amezitaka mamlaka husika kama vile wadau wa afya, menejmenti za maafa, mamlaka za miji na wadau wengine kuchukua hatua stahiki katika kupunguza athari mbaya zinazoweza kutokea katika msimu wa mvua za vuli 2017.

"Wafugaji wanashauriwa kuvuna mifugo yao ikiwa katika hali nzuri kiafya na pia kuvuna maji na wahifadhi malisho ili kukidhi mahitaji katika kipindi cha upungufu," amesema Dk Kijazi.

     

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad