Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wananchi nchini kuendelea kuwa na imani kubwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini katika kulinda Raia na mali zao
Waziri Mwigulu akizungumza kuhusu watu wanaotaka wapelelezi kutoka nje na hatua wanazochukua juu ya watu wasiojulikana.
Waziri Mwigulu amesema kuwa kama yeye ndiye aliyepewa dhamana ya usalama wa Raia na mali zao katika wizara ya mambo ya ndani basi hapatatokea hata kakitongoji kamoja au kauchochoro ambacho kitaonekana kimeshindikana ndani ya nchi yetu, Ameyasema hayo akizungumza na wananchi wa kata ya Kinampanda wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Aidha Waziri Mwigulu amesema kuwa hata watu wanaoshambulia watu watashughulika nao mmoja mmoja hasa waliobeba jina la watu wasiojulikana, kwahiyo wananchi waendelee kuliaamini jeshi la polisi nchini wakati huu ambapo wanaendelea na kazi ya upelelezi wa kuwakamata watu wote waliohusika na mashambulio kwa Mbunge Tundu Lissu, Afisa mstaafu wa jeshi la wananchi na hakimu huko Mtwara kwani uchunguzi huo auna ukomo mpaka upate wote katika idadi yao waliohusika na mashambulizi.
Waziri mwigulu ameongeza kuwa nchi hii ni nchi huru inajitegemea na kuna watu wanasema wanataka vyombo vya nje vifanye uchunguzi, hawa watu wanao fanya uhalifu nchini, upelelezi utafanywa na watu wetu, watakamatwa na vyombo vyetu na watafikishwa katika vyombo vya sheria vya hapahapa tunatakiwa kuamini vyombo vyetu, kama serikali tutashugulikano kwelikweli na si kama hatujaanza nao tunashughulika nao.
Hapatatokea Upelelezi Kutoka Nje Uhalifu Unaofanywa Nchini Utapelelezwa na Vyombo Vyetu- Mwigulu
2
September 26, 2017
Tags
Binafsi napata shida sana na serikali yangu pengine ni uchanga wangu wa mambo ya ulinzi.
ReplyDelete1. Aliuwawa Alphonce Mawazo serilikali kupitia Jeshi la polisi waliendesha uchunguzi mpaka sasa hakuna taarifa.
2. Aliuwawa Dr Mvungi mpaka sasa kimya hakuna taarifa yoyote
3. Alitekwa Dr Ulimboka akateswa mpaka sasa kimya jeshi la polisi halijatoa taarifa
4. Alitekwa mhalili Absom Kibanda mpaka sasa kimya hakuna taarifa ya jeshi la polisi kuhusu tukio hili
5. Alipigwa Risasi na kuuwawa mhadhili chuo kikuu cha Dar Es salaam jina sikumbuki mpaka sasa hakuna taarifa
6. Ben Rabiu Saanane kapotea katika mazingira ya kutatanisha na huku akiwa ametoa taarifa za kutishwa kwake na kuripoti namba ya vitisho hivyo mpaka sasa kimya hakuna taarifa za jeshi la polisi wala usalama
7. Ametekwa Roma mkatoliki na mwenzake mpaka sasa hakuna taarifa ya jeshi la polisi au chombo mingine cha usalama
Na matukio mengine ambayo siyakumbuki. Je kwa tukio la Lisu kupigwa Risasi saa samba mchana kwenye eneo ambalo lina ulinzi wa kutosha polisi watatoa jibu ?
Naona ni vyema serikali ikubali kuleta vyombo huru vya upelelezi na kubaini wahusika maana watu wengi wakiwemo raia wema wa kibiti na viongozi wetu wameuwawa sawa majambazi wengi wameuwawa na jeshi letu, je tu najua chanzo cha mauaji ? Ni vyema tukasaidiwa.
Kusaidiwa sio kuwa tutakuwa tumeshindwa la ila kubadiroshana uzoefu.
Serikali haina sababu ya kukataa kuleta wachunguzi huru maana kuendelea kukataa kutaichafua na kuonekana kama inamkono wake kumbe rahasha
Kama hawa wa ndani wameshindwa, hao 'wanje' ndio wataweza?? Hebu tupeni mifano ya nchi za nje ambazo walileta wachunguzi toka nchi nyingine wakafanikiwa. Hebu msitudanganye, au mnawatafutia 'tenda' nanyinyi mpate 10%?? maana MVUNJA-NCHI-NI-MWANANCHI-NA-MJENGA-NCHI-NI-MWANANCHI.......
ReplyDelete