Hatimaye Mchezaji Hasheem Thabit Apata Timu ya Kuchezea Kikapu nje ya Marekani

Mtanzania Hasheem Thabeet ambaye alikuwa anacheza mchezo wa mpira wa kikapu katika Ligi Kuu ya kikapu ya Marekani NBA, leo September 27 2017 ameripotiwa kujiunga na timu ya kikapu ya Yokohama B-Corsairs inayoshiriki Ligi Kuu ya kikapu nchini Japan.

Hasheem Thabeet ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wa mpira wa kikakupu waliyofanikiwa Tanzania, amewahi kucheza vilabu kadhaa vya kikakupi nchini Marekani amapo ndio nchi inayofanya vizuri kwa upande wa Basketball duniani, Hasheem amepewa jezi namba 34.


Ligi Kuu ya kikapu nchini Japan inatarajiwa kuanza Ijuma hii ya September 29 2017, kama utakuwa unakumbuka vizuri Hasheem Thabeet amewahi kuzichezea timu za Memphis Grizzlies, Portland Trail Blazers na Oklahoma City Thunder, Ligi Kuu ya kikapu ya Japan itaanza Ijumaa ya September 29
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad