Hivi Ndivyo Korea Kaskazini Ilivyoiweka Matatizoni Tanzania


Umoja wa Mataifa unaichunguza Tanzania kwa tuhuma za kikuikwa vikwazo vua kisilaha ilivyoiwekea Korea Kaskazini ambapo inadaiwa kuwa licha ya vikwazo vilivyowekwa, Tanzania imeendeleza biashara ya silaha na nchi hiyo.

Katika ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Septemba 5 mwaka huu imeeleza inachunguza madai ya kampuni ya Korea Kaskazini, Haegeumgang Trading Corporation kuwa inafanyakazi ya kuboresha eneo la kurushia makombora la Tanzania.

Mbali na hiyo, Umoja wa Mataifa umedai kuwa kampuni hiyo inafanyia maboresho rada za ulinzi za Tanzania.

UN imeeleza kuwa, thamani ya mkataba huo wa kijeshi kati ya Tanzania na Korea Kaskazini ambao sio halali ni €10.49 million (Tsh bilioni 28).

Katika ripoti hiyo, UN wameeleza kwamba Tanzania bado haijatoa ufafanuzi kuhusu madai hayo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dr. Suzan Kolimba alisema kuwa hawajapokea taarifa yoyote kutoka UN na hivyo kwa sasa hawawezi kuzungumza kuhusu madai hayo yaliyotolewa.

Mbali na Tanzania, mataifa mengine yanayochunguzwa na UN ni kwa kuendeleza biashara na Korea Kaskazini ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eritrea, Msumbiji, Namibia, Syria na Uganda.

Korea Kaskazini imekuwa ikiwekewa vikwazo mbalimbali siku za karibuni kutokana na kuendelea na majaribio ya silaha za nyuklia kinyume na makubaliano ya UN.

Kiongozi wa nchi huyo, amewahi kunukuliwa akisema kuwa nchi hiyo kwa sasa ina makombora makubwa yanayoweza kulenga sehemu yoyote ya dunia. Moja ya kombora ambalo inadaiwa Korea Kaskazini wanalo, lina uwezo kuliko makombora mawili ya Hiroshima na Nagasaki yakiwekwa pamoja.

Nchi mbalimbali ikiwwamo Marekani na China zimekata au kupunguza biashara na Korea Kaskazini ikiwa ni lengo la kuishinikiza nchi hiyo kusitisha majaribio ya silaha za nyuklia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad