Wataalamu wameeleza kuwa unene wakupita kiasi kwa wanawake husababisha wanawake hao kuwa kwenye hatari ya kujifungua kwa njia ya upasuaji pindi wanapopata ujauzito.
Imeelezwa pia kuwa kesi za watu wanawake kujifungua kwa upasuaji zinaongezeka duniani kote na kutokana na masuala hayo ya uzito mkubwa lakini pia ni hatari wanayokuwa nayo wanawake wanaopata ujauzito kwenye umri mkubwa.
Upasuaji wakati wa kujifungua uko wa aina mbili ikiwa ni pamoja na ule ambao hupangwa mapema hasa kutokana na sababu za kiafya kama mtoto kuwa amelala upande usiotakiwa au mtoto ni mkubwa zaidi wakati upasuaji wa pili ni ule wa dharura ambao hufanyika endapo kuna tatizo wakati wa kujifungua.