Hizi Hapa Sababu za Jeshi la Polisi Mkoani Geita Kumshikiria Mbunge Msukuma

Hizi Hapa Sababu za Jeshi la Polisi Mkoani Geita Kumshikiria Mbunge Msukuma
JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ kutokana na vurugu zilizotokea eneo la Mgodi wa GGM Septemba 14 mwaka huu.
Mbunge Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milion zinazotokana na kodi ya huduma.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo jana alithibitishwa kukamatwa kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini Geita. Kamanda amesema kukamatwa kwa Musukuma ni mwendelezo wa Polisi  kuwakamata watu wote waliohusika katika vurugu zilizotokea Septemba 14.

Amesema tayari wamekamata madiwani wengine wawili na wananchi  watano na kwamba jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi na msako wa kuwakamata wote walioshiriki.
“Bado tunaendelea na msako na hawa ni wahalifu kama wahalifu wengine na sheria lazima ichukue mkondo wake na  Musukuma tumemkamata sio kwamba amekuja mwenyewe ”amesema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad