Idara ya Mahakama Kenya ina 'Tatizo' - Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'.

Alikuwa akizungumza katika hotuba uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini.

Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.

Wameonya kuikabili idara hiyo baada ya uchaguzi

''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari.

Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta katika ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee waliochaguliwa.

Rais huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa.

''Tuna matatizo hapa. Mwanzo ni nani aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe'', alisema.
Amesisitiza kuwa ijapokuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki katika uchaguzi mwengine alisema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na makosa.

''Mahakama ya juu iliketi chini ikaamua kwamba hiyo ndio yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka''.

''Mahakama ya juu haiwezi kufutilia mbali maono ya Wakenya.Na tutaliangazia swala hili.Niangalieni machoni na museme iwapo upendo wangu wa Wakenya kuishi kwa amani ndio unaonekana kuwa uoga, hatuogopi''
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad