IMEBUMA...Waliojifanya Wamelogwa Baada ya Kuiba Gari Mombasa Kumbe Matapeli

IMEBUMA...Waliojifanya Wamelogwa Baada ya Kuiba Gari Mombasa Kumbe Matapeli
KATIKA jiji la Mombasa, kuliibuka kioja cha aina yake siku ya Jumanne baada ya kuonekana  wanaume wawili walioukuwa uchi wa mnyama. Na wote walisemekana kurukwa na akili baada ya kuiba gari la mwanamke mmoja.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Tanzania,  inawaonyesha vijana hao wakicheza kulizunguka gari waliloiba, mmoja wao akiwa amembeba nyoka shingoni, na kundi kubwa la watu likishuhudia kisanga hicho.

Ili kurudishiwa akili zao, mwanamke mganga  alidai dola 1000 za marekani sawa na shilingi 2,300,000 za Tanzania.

 Hata hivyo, baadaye polisi ilibaini kisa hicho kuwa ni uongo uliotengenezwa kwa lengo la kutapeli na kufanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote wanne ambao ni: wanaume wawili waliojifanya kurukwa na akili, mwanamke aliyeibiwa gari, na mwanamke aliyejifanya mganga. Pamoja na makosa hayo, mganga huyo amekutwa na shitaka jingine la kumiliki nyara za serikali bila leseni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad