Imefichuka Sehemu Alipo Dereva wa Tundu Lissu...Hayupo Tanzania..Mbowe Ataja Alipo

Mwenyekiti wa (CHADEMA) Freeman Mbowe amefunguka na kuweka wazi sehemu alipo dereva wa Tundu Lissu ndugu Simon Mohamed Bakari na kusema kwa sasa yupo nchini Kenya akipatiwa huduma za kisaikolojia kufuatia kushuhudia tukio hilo la kinyama.

Mbowe amesema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sakata hilo na kusema kuwa waliona ni busara kumchukua dereva huyo na kuwa naye nchini Kenya kwa ajili ya kupatiwa msaada huo hadi watakapooona hali yake ya kiafya na uhakika na usalama wake ndiyo anaweza kurejea nchini Tanzania.

"Dereva wa Mhe. Lissu, Simon Mohamed Bakari naye tunaye hapa Nairobi akiendelea kupata huduma za kisaikolojia. Alishuhudia shambulio lile na aliokoka kimiujiza. Anasumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Naye hatukuona busara kuendelea kumwacha nchini hadi hapo hali yake ya kiafya na kiusalama itakapohakikishwa. Ni dhahiri kwa aina ya shambulio lilivyokuwa, wauaji walikusudia kuwauwa wote, Mhe. Lissu na hata Dereva wake" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hilo Mbowe amewataka wabunge wa upinzani kuwa na tahadhari kubwa akidai kuwa kama wasipokuwa makini huenda kiongozi mwingine anaweza kupata matatizo kama hayo hata hivyo amesema kuwa tamko la chama chake litakuja karibuni.

"Tutamuenzi Baba wa Taifa aliyetuasa: “tukiwa waoga tutatawaliwa ma madikteta!” Wabunge na Viongozi wa Upinzani ndiyo “Target”. Nawasihi viongozi na wabunge wetu wachukue kila tahadhari. Wanachama nao wawe tayari kulinda na kupigania wajibu wetu, usalama wa viongozi na chama chetu kwa ujasiri. Tusipochukua hatua, kesho atadhurika mwingine!Tamko na agizo rasmi la Chama litafuata karibuni" alisema Freeman Mbowe.

Freman Mbowe amedai kuwa Tanzania si sehemu salama tangu umefanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kudai kuanzia hapo yalianza kujitokeza kwa mauaji ya viongozi kikiwepo kifo cha Mhe. Alphonce Mawazo Mkoani Geita, Kupotea kwa kina Ben Saanane. Kutekwa  wasanii na kufanyiwa mateso makubwa pamoja na Wabunge kufungwa na kushtakiwa kila siku.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Too bad Mhe mbowe u don't have to be one sided in such issues.
    Those people killed in kibiti weren't they human beings?au kwa sababu walikua sio wa CHADEMA
    Sometimes u need to think like a leader not as an opposition leader

    ReplyDelete
  2. Kwa tabia aliokuwa akienda nayo Tundu Lisu sio nzuri hata kidogo kwani kiburi ni jambo baya kwa mwanadamu. kauli zake za kama .....nitanyamaza labda nikifa. Dikteta uchwara. Na tabasamu za dharau katika mihimili ya dola kama mahakama na vyombo vya usalama ni dhahiri ilikkuwa sio ushujaa bali ni upuuzi wa hali ya juu aliokuwa akiuonyesha. Kiongozi wa nchi mara zote anakuwa sio yeye mwenye madhara wenye madhara ni wale waliemuamini ili awe kiongozi wao. Unapoamua kupambana au kuleta dharau kwa kiongozi wa nchi jua yakwamba kuna uwezekano mkubwa yakwamba kuna watu unawaumiza zaidi kuliko kiongozi mwenyewe na si ajabu wakakukurudi. Mbaya zaidi licha ya yeye mwenyewe Lisu na wapambe wake kujitapa kuwa anapigania haki lakini kuna mambo kadhaa aliokuwa akiyapigania Lisu imewafanya baadhi ya watanzania kutokwa na imani nae tena na kuridhirika kabisa yakuwa Lisu ni mnafiki na Msaliti wa nchi yao na pengine ni kibaraka pia. Tabia ya Lisu pengine na washirika wake wa upinzani kupinga wazi wazi hatua kadhaa zinazochukuliwa na serikali za kimaendeleo zinawakera wananchi waliowengi. Suala la mchanga wa dhahabu ambapo Lisu alikuwa yupo against nalo kupatiwa ufumbuzi limemuweka Lisu kwenye utata mkubwa. Hata sherehe yake ya kuwaalika wanahabari kuwaarifu kuzuiwa kwa Bomberdier kuna baadhi ya watanzania wametafsiri na pengine ndivyo ilivyokuwa yakwamba Tundu Lisu aliwaita waandishi wa habari kufurahia ushindi wake zidi ya Maghufuli kushindwa kuileta ndege hiyo hapa nchini kwa wakati. Kwa tabia aliokuwa anakwenda nayo Tundu Lisu nchi yeyote duniani pale angejikuta kwenye matatizo. Huko ulaya ndio kabisa wananchi wake ni very understanding mtu kama Lisu wangekuwa walishampoteza kisiasa yeye na chama chake. Inasikitisha sana yaliyompata Tundu Lisu lakini panapo ukweli lazima tuambieni ukwel Tundu Lisu ni mtu mwenye kiburi na kama vile alikuwa hana washauri au alikuwa hashauriki. Watu watabaki kulaani na kumtafuta mchawi kwa aliyoyapata lakini ingekuwa vizuri jitihada zingefanyika kumshauri na kumuepusha na maafa aliyoyapata. Watanzania wapo serious hivi sasa katika vita vya uchumi na wanamuamko na hamasa za ajabu kwa hivyo ni rahisi sana kwa mtanzania yeyote kupambana na kitu chochote kile chenye ishara ya kuwaletea pingamzi katika harakati zao za kimaendeleo ikiwezekana hata kuchukua maamuzi ya kipumbavu. Nchi ambayo raia wake wanatoboana macho mchana kweupe mpaka kusababisha upofu kwa mtu mwengine vipi tunashagaa la Lisu au kwakuwa mwanasiasa? Mwanasiasa ni mwananchi pia wanatakiwa kuwa na adabu ili kujiepushia na maafa. Serikali ni Serikali ni jalala kila mwenye taka zake anatupa ila sio taka zote zimezalishwa na serikali. Kuna ushauri alipewa Nabii Mussa na M/Mungu wakati alipoamriwa kurudi misri kumkabili Firauni na kuwakomboa wana wa Israel. M/MUNGU alimkumbusha nabii Mussa kua na busara wakati akimkabili Firauni hasa pale atakapomueleza kuwa yeye Firauni sio Mungu kuna Mungu wa kweli. M/Mungu alimtabanaisha Nabii Musa yakwamba licha ya udhalimu wa Firauni lakini ni kiongozi wa nchi na mwenye mamlaka kwa hivyo heshima lazima iwepo licha yakuwa Nabii Mussa alishabashiriwa ushindi na M/Mungu. Kwa kifupi no one can fight Government and win except Government otherwise hes looking to harm himself.

    ReplyDelete
  3. Wadau wote wawili hapo juuNAKUBALIANA NANYI KWA ASILI MIA MOJA.
    MMEZINGUMZA YA MAANA NA UKEELI KABISA.
    HESHIMA NA ADABU NI KITU CHA BURE.
    LEO MTU AKAE AJIONE UEYE NDITE KAPEWA ULIMI NA AUTUMIE ANAVYOTAKA KUKERA NA KUBEZA JUHUDI ZINAZO CHUKULIWA KUINYIOSHA NCHI HII NA KULINDA RASILI MALI ZETU SISI ZAIDI YA MAMILIONI HAMSINI. KWA VIJITU AU KIKUNDI CHA WSPINGA MAENDELEO NA WENGINE KUANZA KIJITABIRIA MAJANGA NA HAPO HAPO NDANI YAKE HIVYO VIKUNDI VINA UHASAMA NA USAFISHIANANAJI WA HESABU.
    LISU AMEWAKERA WENGI HATUFURAHII YALIYOMPATA ILA KWA KIASI KIKUBWS AMECHANGIA MWENYEWE KWA KUJIFIKIRIA AU KUONA YEYE NI LAMBO WA MITAANI NA MAGAZETINI NA KUSAHAU SLVESTER STALLONI ALIKUWA NII ACTION MOVIE NA SI KWELIHATAUKIANGALIA RAMBO2 BEHIND THE SCENE UNAELEWA NA KUONA KUWA ANALIPWA .
    Tumuombee apone. Anaweza kuja kutubu. Na mjomba razi Watanzania na kushiriki ktk ujenzi WA Taifa.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA UDUMUAHE UPENDO NA AMANI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad