Jeshi la Polisi: Askari wa Interpol Aliyekuwa Nairobi Alikuwa Kikazi, si Kama Inavyosambazwa Mitandaoni

Msemaji wa jeshi la Polisi Tanzania,Kamishna msaidizi Barnabas Mwakalukwa ameongea na kutoa taarifa kuwa,askari wa Interpol ambaye picha yake imesambaa mitandaoni kuwa ameonekana katika viunga vya Nairobi alisharudi nyumbani Tanzania.

Askari huyo alitiliwa mashaka sababu ya uwepo wa Tundu Lissu hospital Nairobi,na picha zake zilisambaa kwa kasi mitandaoni.

Msemaji wa Polisi anasema,askari huyo ni kweli alikuwepo Nairobi toka tarehe 04/09/2017 hadi 08/09/2017 kwa ajili ya mafunzo maalumu,na alirudi siku kadhaa zilizopita baada ya kuwa amemaliza mafunzo hayo.

Hivyo ni kweli alikuwa Nairobi,lakini si kwa kuhusishwa na tukio la Tundu Lissu,bali alikuwa kwa shughuli za kikazi ambazo amekwisha maliza na kurudi Tanzania.

Taarifa za uwepo wa "kachero" huyo katika viunga vya Nairobi,zilianza kusambaa kupitia account ya mtandao wa Tweeter wa Mbunge Halima Mdee,akisema kuwa wamepata taarifa za uwepo wa askari huyo na wanafuatilia nyendo zake katika jiji la Nairobi,maana inadhaniwa ametumwa kwa "kazi maalumu"

Jeshi la Polisi limeomba Wananchi kutokusambaza tena ujumbe huo baada ya ufafanuzi huo,na yoyote atakayeusambaza,atakuwa anatenda kosa la jinai na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Msikilize hapa chini msemaji wa Jeshi la Polisi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad