Kampeni ya 'Fataki' la Kuongeza Uelewa wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kuanzishwa Tena

Kampeni ya 'Fataki'  la Kuongeza Uelewa wa Maambukizi
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) iko mbioni kurudisha kampeni za ‘Tuko wangapi’ na ‘Fataki’ ili kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, Jumanne Issango amesema miaka ya nyuma kampeni hizo ziliendeshwa kwenye vituo vya redio na televisheni lakini hazikuendelea kutokana na upungufu wa rasilimali fedha.

“Fedha zilizokuwa zikitumika kuendesha kampeni si endelevu kutokana na wafadhili kuja na baada ya muda wao kuisha wa kufanya kazi nasi huondoka na kuacha pengo,” amesema.

Amesema watazirejesha kampeni hizo kutokana na kuwepo mazungumzo na wafadhili ambao wameona mchango wake katika kupiga vita maambukizi ya VVU.

Issango amesema kurudi kwa kampeni hizo kutaenda sambamba na utafiti wa mwenendo wa Ukimwi nchini wa mwaka 2016/17 mwishoni mwa Novemba.

Amesema kuna dalili kuwa maambukizi mapya ya VVU yanapungua katika jamii kupitia utafiti huo.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema semina na kampeni zinazoendeshwa kitaifa za kuzia maambukizi ya Ukimwi zimechangia  kupunguza maambukizi mapya.

Amesema mkakati huo unalenga kupunguza nusu ya kiwango cha maambukizi mapya ya VVU kutoka asilimia 0.32 mwaka 2012 hadi 0.16 mwaka 2018 pia kupunguza kiwango cha vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Issango amesema wameongeza wigo katika utafutaji takwimu kwa kuwatumia watoto kuanzia umri 0 hadi miaka 49.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad