Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu

Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu
Nimepata taarifa ya Acacia kupunguza shughuli zake BULYANHULU na hivyo kuleta tiahio la madhara ya kiuchumi kwa wafanyakazi zaidi ya 1,200; wakandarasi zaidi ya 800 na wananchi kaka maelfiu Kakola na maeneo jirani. Hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi.

My immediate reaction kwa hali hii ni KUIOMBA SERIKALI IRUHUSU WANANCHI AMBAO NI WACHIMBAJI WADOGO KWA MAISHA YAO YOTE, WAANZE KUCHIMBA REEF 2 na maeneo mengine yenye madini ndani ya leseni ya Acacia pembeni ya mgodi ili maisha yaendelee.

Ni vema pia seriklai ikasimamia kuhakikisha haki za wananchi, hasa wafanyakazi na wakandarasi wenye mikataba zinalindwa wakati huu. Serikali isiwaache wafanyakazi wakafanyiwa anachopenda mwekezaji. Ni muhimu SERIKALI ifanye hivyo ili wajue there are consequences for any action they take.

Nawasihi wananchi wangu (hasa wafanyakazi, wakandarasi na wengine ambao wamepata madhara ya moja kwa moja) tuendelee kuwa watulivu tukiamini Mazungumzo yanayoendelea kati ya SERIKALI na Barrick yatapelekea haki zetu zilizoporwa siku zote kurejeshwa na neema endelevu kupatikana.

Mawasiliano rasmi kati ya ofisi yenu (ya Mbunge) na SERIKALI kuhusu maombi mnayopenda SERIKALI iyafanyie kazi kwa jinsi mambo yanavyokwenda yanafanyika.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MWEKEZAJI MAGUMASHI ALIWATUMIA WATANZANIA (WAJALI MATUMBO YAO) NA KUKOSA UADILIFU NA UZALENDO WAKASHIRIKIA NAO KUIANGAMIZA NCHI NA KUICHUKUA MALI ASILI KAMA TOKA SHAMBA LA BIBI MPAKA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA( USALAMA ) KUHAKIKISHA WANAIBA VIZURI WAKISINDIKIZWA RASMI MPAKA KUZIVUSHA KATIKA VYOMBO MAJINI NA VIWANJA VYA NDEGE MACHIMBONI . ONONGO BAKALI MPACHU. TUTAKUTAIFISHENI NA KUFUNGA AKAUNTI ZENU ZA NJE NA UWEKEZAJI WENU KWA MAJINA YA JAMAA ZENU.
    BADO TUKO KAZINI NA MASILAHI YETU YOTE TUNAYAZUNGUMZIA HAKIPOTEI KITU NA MALIMBIKIZO NA KODI ZOTE ZITATOKA TUU. BULYANHULU NA BUZWAGI ZIKO WAPI?????? ( TANZANIA ) NA TANZANIA YA NANI??? YA WATANZANIA NI MIMI NA WEWE TUJENGE UZALENDO NA UPENDO. TUTAWASHINDA NA MBINU ZAO ZA UJANJA UJANJA.

    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad