Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amefunguka na kudai atamkumbuka aliyekuwa rais mteule wa nchi ya Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kuweza kuwa mtu wa kidemokrasia wa dunia katika zama za sasa.
Ridhiwani Kikwete ameeleza hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa twitter mapema leo baada ya Mahakama ya Juu nchini Kenya kutengua matokeo ya uchaguzi mkuu upande wa rais nchini humo kutokana na Tume ya Uchaguzi IEBC kukiuka Katiba na Sheria ya uchaguzi.
"Utakumbukwa kama mtu wa kidemokrasia wa dunia katika zama zetu, hiyo ni ukweli na ninakuombea", aliandika Ridhiwani Kikwete.
Pamoja na hayo, Ridhiwani Kikwete aliendelea kwa kusema "niliwahi kusema najifunza jambo kutoka Kenya, leo imethibitika wakati Mahakama inafungua kurasa mpya ya kumbukumbu ya maamuzi", alisisitiza Ridhiwani Kikwete.
Huu hapa chini ndiyo ujumbe wa Ridhiwani Kikwete aliouandika kuhusiana na maamuzi ya Kenya yaliyotolewa na Mahakama ya Juu nchini humo.
Maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Juu nchini Kenya leo Septemba mosi yameweza kusimua hisia za watu wengi duniani kwa kila mmoja kuwa na mawazo tofauti juu ya tukio hilo lililoweza kuwa la kihistoria nchini humo.