Kimbunga Irma Chaikumbu Cuba
0
September 09, 2017
Kimbunga kikubwa kilichopewa jina la Irma kimeipiga nchi ya Cuba na kusababisha vifo baadhi ya maeneo mengine, huku kikiharibu miundo mbinu ya nchi hiyo.
Kimbunga hicho ambacho kimeendelea kuimarika kinatarajiwa kuathiri miji ya pwani, na mpaka kufikia sasa watu 22 wameripotiwa kufariki katika visiwa vya Carebean.
Pia katika jimbo la Florida nchini Marekani watu milioni 5.6 ambao ni sawa na 25% ya watu wa maeneo hayo, wametakiwa kuhama makazi yao kujinusuru na kimbunga hicho kikubwa.
Kimbunga hicho kinakadiriwa kwenda spidi ya km 249 kwa saa, pia kimesababisha mvua kubwa na mafuriko, katika maeneo ambayo kimepita, huku kikisababisha watalii kukimbia nchi ya Cuba, na maelfu ya watu kukosa makazi.
Katika eneo la Berbuda takriban 95% ya majengo yake yameharibiwa hasara inayokadiriwa kufikia dola milioni 100.