Kodi ya Nyumba Yamrudisha Mainda Nyumbani Kwao

Mange Kimambi Atajwa Mhamasishaji Bora wa Kuchangisha Fedha ya Matibabu ya Lissu
STAA wa Filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ juzikati alizua timbwili nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni jijini Dar alipotembelewa na waandishi wetu waliotaka kujua ukweli wa madai kwamba, eti kaamua kurudi kwao baada ya kukosa kodi ya kulipa huko alikokuwa akiishi.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia ubuyu uliovujishwa na sosi wetu aliyedai kuwa, mwanadada huyo kwa sasa mambo yake siyo ‘mswano’ kama ilivyokuwa huko nyuma na ameamua kwenda kuanza moja nyumbani kwao.
MSIKIE SOSI
“Hivi mnajua kuwa Mainda karudisha mpira kwa kipa? (Kaenda kuanza moja kwao) Kama hamjui basi habari ndiyo hiyo, fuatilieni licha ya kwamba mwenyewe hataki watu wajue wala wamtembelee,” kilidai chanzo hicho.
RISASI LATINGA KWAO
Baada ya kuinasa habari hiyo, mapaparazi wetu juzi Jumanne walitinga nyumbani kwao ili kupata ukweli ambapo walimkuta Mainda na kuongea naye.
ALIAMSHA DUDE, MSIKIE…
“Mmekuja kufanya nini hapa nyumbani? Mbona mimi sihitaji waandishi hapa, mimi sio staa tafadhalini na wala sihitaji kuongea na waandishi, kwanza mmekuja bila taarifa,” alisema Mainda kwa sauti ya kufoka.
Alipobanwa sababu za kuwepo nyumbani kwao alisema yupo pale kwa ajili ya kumuuguza mama yake mdogo ambaye aliyejifungua kwa upasuaji.
AZUA TIMBWILI
Aliporushiwa madai kwamba yupo pale kwa sababu ya kukosa kodi huko alikokuwa akiishi, staa huyo alianza kuongea kwa jazba kabla ya kuliamsha timbwili akiwataka waandishi kuacha kufuatilia maisha yake.
“Jamani nilishawaeleza kuwa mimi sitaki, naomba muondoke haraka sana, mimi kuja kwetu kuna ajabu gani sasa? Kwani nakatazwa? Hata kama nimekosa kodi nyinyi linawahusu nini?
Niacheni jamani,” alisema Mainda ambaye alikuwa akiongea kwa sauti hadi kuwafanya watu wajazane eneo hilo. Kufuatilia hali hiyo, waandishi wetu waliamua kuwa wapole na kuondoka nyumbani kwa staa huyo ili kuepusha shari.
NENO LA MHARIRI
Gazeti hili linamuomba Mainda kuwa mpole huku akiweka akilini mwake kuwa kukosa leo siyo kukosa kesho na tunamuombea apate kile anachokihitaji. Endapo watu wanazusha yale yanayosemwa ni vyema akatoa ufafanuzi kama staa kuliko kuibua shari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad