Kubenea Ashindwa Kuhojiwa na Kamati ya Bunge Alazwa Katika Zahanati ya Bunge

Kubenea Ashindwa Kuhojiwa na Kamati ya Bunge Alazwa Katika Zahanati ya Bunge
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amepelekwa katika zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya.

Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Jumatano kuwa, Kubenea amefika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na amewaeleza kwamba hali yake si nzuri.

Kutokana na hilo, amesema amepelekwa kwenye zahanati hiyo na hali yake itakapoimarika atahojiwa na kamati.

Mbunge huyo ambaye alipelekwa Dodoma kwa ndege leo asubuhi, jana Jumanne alisema alikuwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay  wilayani Kinondoni akisubiri utaratibu wa safari hiyo ya kwenda kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mfyuuuu!! afya mbovu, mdomo mrefu kama chupa, unataka kufia mikononi mwa watu useme umeuwawa.....msonyoooooooooooooo

    ReplyDelete
  2. Weee hspo juu ni kati ya watanzsnia wengi sugu smmbao hata watu wakitetea haki ni yenu cdm. Mmeiweka ccm mbele mko tayari watu kama kubenea wafe kwa kusapoti chsma, kundi, hata raisi bila kujsli ni Tanzania, nchi na jamii ndio iumiayo. Badala ya kutoa hoja unamshambulia mtu kimaumbile. Ni ujinga usiofundishika kwa wengi wstanzsnia kisa uhaba wa akili, uduni wa kufikiri, na kutokujikomboa kiuzalendo. Mtu mmoja hawezi kubadili Tsifa. Mpska watsnzsnia wengi watakapokuwa tayari kukikomboa kielimu, kifikra, kiutendaji. Wengi mnamtegemea raidi ambaye si mtendaji. Mmezoea kuamriwa, uhuru wenu nguvu zenu , majukumu yenu hamyajui hata.maendeleo yataletwa na watu watakapojitambua ni wao ndio wenye majukumu, waamuzi, wapanga maendeleo ya kwao waonavyo. Na si raidi aamuavyo vipi mambo yafanyike. Na si wachina wanapopewa uhuru nchini kufanya wspendavyo wakiwa di wazalendo. Ambapo wazalenfo wanapopigania haki wanafungwa na kuteswa. Mnakubali wawekezaji wezi, halafu wanapoiba mnalalamika. Mkiambiwa sheria mbovu, na mfumo mbovu, mnawaweka ndani. Mkiambiwa maneno mengine raisi asemayo hadharani yanalitenga taifa, ya kiubaguzi kichama, mnawsnyanyasa, ni mtu kama wewe hapo juu unatoa utumbo bila kufuatilia hoja nzito zinazotukabili nchi yetu. Ni ujinga, upumbavu, udiofundishika. Na ujinga huu nfo unaleta hii ditomfahamu sababu mnaikubali amri. Mmzoea amri, badala ya mijadalaya wote watsnzsnia kujadili kwa nini nchi ipo hivi kwa sasa. Ningelikuws wewe ningeomba mikutao ya wazi kulixungumzia hili. Watanzsnia eote bila kujali dini, chama jinsia na cheo.ndipo tutaleta maendeleo ya kweli na tunayoyataka wenyewe na si raisi, wala polsi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad