Maafisa Ardhi Waliogawa na Kuuza Viwanja vya Polisi Kukamatwa

Maafisa Ardhi Waliogawa na Kuuza  Viwanja vya Polisi Kukamatwa
Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Fadhili Nkurlu amemuagiza Mkuu wa Upelelezi wilayani Kahama, George Bagyemu kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maofisa ardhi waliogawa na kuuza viwanja vilivyopimwa na kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi.

Mkuu wa Wilaya huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama amesema hayo leo baada ya kutembelea na kuona jinsi ambavyo maafisa hao wa ardhi walivyoweza kuuza robo tatu ya eneo la chuo cha maendeleo jamii Kahama likiwa limeuzwa kwa watu binafsi na kujengwa nyumba.

Katika hatua nyingine fadhili Nkurlu amemuagiza mfanyabiashara maarufu wilayani Kahama aliyeuziwa eneo la polisi Bw.Jeremiah Ndasa pamoja na wengine kuvunja ukuta na misingi ya nyumba wayojenga katika eneo hilo na kuliacha wazi kwa matumizi ya serikali.
Aidha Mkuu wa Upelelezi wilayani Kahama, George Bagyemu amesema maeneo yote ya polisi yaliovamiwa na kujengwa yako katika ramani huku Afisa Ardhi mteule Kahama Bw.Yusuph Shabani akijitetea mbele ya mkuu wa wilaya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad