Maafisa Utumishi Watakaochelewesha Mishahara Kukiona
0
September 07, 2017
Serikali imetangaza kiama kwa maofisa utumishi wote ambao watachelewesha mishahara kwa watumishi bila sababu za msingi.
Aidha, katika uwajibikaji huo, Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na manispaa watakuwa wakifungiwa mishahara yao kama itabainika katika maeneo yao kuna watumishi wanacheleweshewa mishahara.
Onyo hilo limetolewa leo bungeni na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki wakati akijibu swali la nyongeza na Innocent Bashungwa (Karagwe-CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua serikali inawaambia nini watumishi ambao wamekuwa na uzembe katika kubadilisha mishahara ya watumishi ambao wanastahili na wakati mwingine kuchelewesha mishahara hiyo.
"Katika hili hatutakuwa na huruma na mtumishi yeyote kama tulivyofanya kwa baadhi ya maofisa na ndivyo tutakavyofanya na tumeamua kwenda mbali zaidi kwa kupanga kufungia mishahara wakurugenzi ambako maeneo yao kutokea mkanganyiko huo," amesema Kairuki
Kuhusu malimbikizo ya watumishi wanaodai kwa ajili ya nauli nyakati za likizo, amesema kiasi cha Sh 1 tririoni zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa watumishi hao baada ya kukamilisha kuhakiki madai yao.
Tags