Zaidi ya watu 600 wamehama wakati wa makabiliano ya siku ya Jumanne katika miji iliyo mashariki mwa nchi
Waandamanaji wanawalaumu polisi kwa kutekeleza mauaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu dhidi ya watu wa Oromo.
Serikali imesema kuwa ghasia hizo zimesabaishwa na mzozo wa mpaka kati ya watu wa Oromo na majirani zao walio eneo la Somalia nchini Ethiopia
Serikali imesema kuwa sasa imetuma jeshi kwenda kufanya kile kile ilichokitaja kuwa kutwaa silaha
Mzozo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa lakini umechaha wiki hii na kugeuka kuwa makabiliano makali.
Mwezi Agosti serikali iliondoa amri ya tahadhari iliyowekwa kufuatia maandamano ya zaidi ya miaka miwili yanayoipinga serikali.