Maaskofu Nao Waanza Kuweweseka Mgao wa ESCROW, Kilaini na Eusebius Wamerudisha Mgao Waliopewa

Askofu Msaidizi jimbo la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini pamoja na Mhashamu Eusebius Nzigilwa wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam wamefunguka na kutoa taarifa kuwa wameamua kurudisha mgao wa fedha za Escrow ambazo walipewa na James Rugemalira.

Viongozi hao wa dini wamesema wameamua kurudisha fedha hizo za serikali kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani ya kuhujumu uchumi inayomkabili James Rugemalira ambaye ndiye aliwapa fedha hizo.

Mhashamu Method Kilaini alidaiwa kupewa jumla ya fedha za kitanzania milioni 80.5 huku Eusebius Nzigilwa akidaiwa kupewa jumla ya milioni 40.4

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duhhh Nchi Itanyooka tu

    ReplyDelete
  2. BINAFSI SIONI SABABU YA KURUDISHA KAMA ZILITOLEWA KAMA SADAKA KANISANI!!

    ReplyDelete
  3. hIVYO binaadamu mpaka unapewa na kupokea Pesa ambazo hujui uhalali wake na sababu yake unachukua.
    Hivyo hujiulizi na kushtukia hilo????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad