Rais John Pombe Magufuli ambaye leo Septemba 20, 2017 yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro amefunguka na kumsifia Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya na kusema ni mbunge mchapakazi.
Rais Magufuli amesema Ole Millya ni mchapakazi kutokana na ukweli kwamba mbunge huyo amelelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukulia ndani ya chama hicho hivyo sasa yupo CHADEMA lakini moyo wake ni CCM.
"Miliya ni mchapakazi, kwa sababu amelelewa na CCM, unaweza kumuona ni CHADEMA lakini moyo wake huyu ni Chama Cha Mapinduzi (CCM)" alisema Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa Mungu huenda alikosea kuipa Tanzania madini ya Tanzanite kwani madini hayo yamekuwa yakiibiwa huku Watanzania wenyewe wakishindwa kunufaika na mapato ya madini hayo.
"Mungu alifanya makosa alileta Tanzanite kwa Watanzania, lakini kama hakufanya makosa basi tubadilike jinsi ya kutumia Tanzanite. Tanzanite ingekuwa inatumika vizuri kusikungekuwa na tatizo la barabara hapa Simanjiro, hapa Simanjiro msingekosa hata Ambulance moja lakini kwa kuwa hamna gari hata moja ya wagonjwa basi mimi nitaleta gari ya wagonjwa hapa nitajua nifanya nini, nitawakata kata huko tutapata gari" alisema Rais Magufuli.
Kichwa kimoja hakiwezi kuleta maendeleo, bali Watu na ukiwapa uhuru wao wa kufikiri, kuamua, na kutenda watakayo, kwa ajili yao, na kuwasikiliza, kuwaunga mkono, na kuona matakwa yao yanatimia, Ndio kazi ya Kiongozi bora. Ni watu na matakwa yao.Wengi wa Chadema wako hivi. Tena wengi sana zaidi ya huyu. Ungana nao, wanapokuletea hoja, na mawazo yao, ni kuyasikiliza, uwaite mezani, jenga urafiki nao muungane kuwatumikia watu. Ndivyo inavyotakiwa.Hii itajenga Undugu tulioupoteza, itajenga umoja, itaunganisha nguvu, upendo na kutoa woga wa kukuogopa vipi utawachukulia.Amani itawale mioyoni mwetu kufanya haya. Kama wote tunaamani wote tutaelewana, sikilizana, kosoana na mwisho kuafikiana. Lakini si kuwatupa watu jela. Si kuafuatilia. Si kuwashambulia. Si kuwaita maadui.Unamhitaji kila mtanzania kulikomboa Taifa kama unatarajia kuiona Tanzania inasonga mbele kwa amani. Ni kuwaamini Watanzania na kujenga uzalendo. Ni mzalendo tu ataleta maendeleo Tanzania na si mwekezaji wa nje, yeye ni mzalendo kwao. Anakuja kujiongezea utajiri nyumbani kwake si hapa Tanzania. Ukiamini hivi utajenga uhusiano mzuri kwanza na Wazalendo wote kwanza kukiri makosa yaliyotoke. Kuyatambua makosa hayo. Kuangalia nani kayaleta na kwa njia zipi na kuzifunga njia hizo. Pili kutoa adhabu kubwa kwa wahusika bila kujali cheo. Ni hapo tu utakomesha. Lakini kuwakomesha wanaofichua si suruhishi huku wenye makosa bado wamekalia utajiri, vyeo. na Wanasauti kubwa katika serikali yako. Haya ndiyo yanayotikisa Taifa letu kwa sasa.Ukweli unaua wasio na makosa.
ReplyDelete