RAIS John Magufuli ameelezea jinsi ofi si yake ilivyotumia mbinu ya ukachero na uchunguzi na kupata taarifa zote za namna rasilimali mbalimbali za madini ikiwemo dhahabu, almasi na tanzanite zinavyoibwa nchini.
Pamoja na hayo, amebainisha kuwa serikali yake haiko tayari kutishiwa na mtu yeyote anayetumia rasilimali za Watanzania kwa manufaa yake binafsi, na kwamba iko tayarikusimamisha migodi yote isichimbwe kuliko kuruhusu madini hayo kuvunwa na kunufaisha wachache. Dk Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam Ikulu jana wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti mbili za Kamati za Bunge zilizoundwa na Spika Job Ndugai kwa ajili ya kuchunguza biashara za madini ya tanzanite na almasi.
Alisema kabla ya kuunda kamati mbili za kuchunguza makinikia ya dhahabu mapema mwaka huu, tayari ofisi yake ilishafanya utafiti kwa kutumia mbinu mbalimbali na kupata taarifa yakiwemo mawasiliano ya namna ya kuiba rasilimali hizo. “Wakati nikianza kuzungumzia masuala ya wizi, wapo wengine waliona ninazungumza tu kutoka hewani, nataka niwaeleze tumefanya research ya kutosha, tulitumia baadhi ya wafanyakazi, forensic investigation, mfano kwenye dhahabu tuna information zote,” alieleza Dk Magufuli.
Alisema kupitia mbinu mkakati hizo, walifanikiwa kufyonza data za kwenye migodi yote, na hata wahusika waliposhtuka na kubadilisha kompyuta zao walikuwa wameshachelewa kwani taarifa zao zote zilikuwa zimedukuliwa. “Tuna communication zao zote, nataka niwaeleze Watanzania mjue, walivyokuwa wanawasiliana, walivyopanga mikakati ya kuiba, wakishirikiana na watendaji wengine Watanzania, tuna information zote.
Tulitumia watu wetu,” alisisitiza. Alisema wako Watanzania wazalendo, waliotumia nafasi zao wakiwemo baadhi yao walionekana kama wachimbaji, maaskari na hata wenye vyeo vikubwa ambao kazi yao ilikuwa ni kukusanya taarifa kamili za namna wizi unavyofanyika. “Tumekuwa tukitumia maisha ya baadhi ya Watanzania katika kupata taarifa stahiki. Mfano hili suala la tanzanite, nimeambiwa kuna video kwenye flash, lakini mimi ninayo yangu, nimekaa nayo kwa muda mrefu kutoka kwa Watanzania wanaofanya kazi kizalendo kwa ajili yetu,” alisema.
Aliongeza: “Mwingine unaweza ukamuona ni mchimbaji tu, mlinzi, wanatumia mbinu mbalimbali kama kwenye vita. Hii ni vita na ndiyo maana hata askari wanapokuwa kwenye vita, hutuma mashushu wao kwenye vikosi vya maadui,” Alisema katika vita, askari hutuma askari wao kwa upande wa adui na askari hao hulazimika kupigana kwa upande huo kwa lengo la kuaminiwa ili wapate taarifa kamili na sahihi ingawa kwa kufanya hivyo maisha yao huwa hatarini hasa pale wanapobainika.
“Asipoangalia anaweza akauawa na watu wake, mpaka pawe na mtu ayakayesema jamani huyu ni mtu wetu, na anaweza kutambulishwa hivyo akiwa tayari ameshakufa. Nawaambia ukweli katika mchakato huu wapo wenzetu tuliowatuma,” alibainisha. Alisema katika mbinu hizo za kupata taarifa siku tano zilizopita, serikali ilikamata almasi yenye kilo 15.5 ikiwa imegawanyika katika madaraja matatu na inayodaiwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 14.
Hata hivyo, kupitia Watanzania hao wazalendo waliowekwa huko na serikali, baada ya kuzipima na kuzithaminisha, almasi hizo katika daraja la kwanza pekee linalodaiwa kuwa na kilo nne, mpaka juzi zilipopimwa zilibainika kuwa zaidi ya kilo nane. “Sasa hapo bado class ya pili na ya tatu, nina imani kabisa hiyo thamani inayodaiwa ya Dola za Marekani milioni 14, ikawa zaidi ya Dola za Marekani milioni 20 hadi 25. Jambo la kusikitisha Wizara ya Nishati na Madini ambayo ni msimamizi hata vifaa vya kuthibitishia madini hayo kabla hayajasafirishwa haina,” alisema.
Alisema endapo hali hiyo itaendelea ya wizara kukosa vifaa stahiki vya kupimia madini kabla hayajasafirishwa ni sawa na kupigana vita na kumuomba adui unayepambana naye silaha. “Mtashangaa anayeifanya hiyo kazi, aliyevumbua hayo mabaya, anayetupa information zote za kule mpaka tukajua tulikuwa tunapigwa vibaya ni Profesa Mruma (Abdulkarim). Alikuwa ni askari tuliyempeleka kule,” alibainisha Dk Magufuli.
Wakati akiwasilisha matokeo ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi, Mwenyekiti wake, Mussa Azzan Zungu alimtaja Profesa Mruma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kuwa ni mmoja wa watendaji wa serikali ambao hawakuwa makini na kuisababishia hasara serikali.
Alisema Profesa Mruma ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Madini nchini, aliisababishia hasara nchi kwa kuruhusu madini hayo ya almasi yapotee kwa uzembe. Hata hivyo, Dk Magufuli alimtaja msomi huyo kuwa ni mmoja wa wazalendo waliojitolea kama askari na kufanya kazi kama sehemu ya adui kwa faida ya nchi yake.
Akizungumzia maendeleo ya mazungumzo baina ya wawekezaji wa madini ya dhahabu nchini wa Kampuni ya Acacia na serikali, Dk Magufuli, alibainisha kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri tofauti na maneno yanayozungumzwa mitaani. “Nataka niwahakikishie kuwa wapo Watanzania wazalendo wanaofanya kazi kwa ajili ya nchi yao.
Ndiyo maana hawa wazungu wa dhahabu wapo hadi leo wanazungumza, walikuja 14, lakini mpaka leo wameongezeka na kufikia 25, wanaenda kule wanajaribu wanaongezeka, sisi idadi ya watu ni wale wale,” alieleza. “…Nimesikia wengine wanatishia kufukuza wafanyakazi, nilitamani waseme wanaondoka, wakiondoka tutachukua wananchi wa kawaida watajazana mle kuchimba madini. Wao watafukuza 200, tukiruhusu wananchi wetu tutangeneza ajira milioni moja, hii ni rasilimali yetu,” alisisitiza.
Aliwaonya wawekezaji hao wasijaribu kuitisha serikali bali wao ndiyo wajiandae kutishika. Alisema fedha zinazoibiwa kupitia madini ni nyingi kiasi kwamba huenda Tanzania ndiyo ikawa inafadhili nchi zilizoendelea badala ya yenyewe kufadhiliwa. “Sisi tunatengeneza bajeti ya Sh trilioni 20 hadi 30 wao wanachukua Sh trilioni 600, wanakuja hapa wanasema wao ndiyo wafadhili, sisi ndiyo wafadhili,” alieleza.
Alisisitiza kuwa muda wa Tanzania kuchezewa na kuibiwa umekwisha kwani Watanzania wengi wanaishi maisha ya kimaskini, miundombinu mibovu, huduma muhimu kama elimu na afya hazipatikani ipasavyo, huku fedha nyingi zikipotea. “Ukiangalia maeneo ya machimbo au karibu na mgodi wowote wa dhahabu au tanzanite unaweza kuona maisha ya wanaoishi karibu na hiyo migodi.
Angalia maisha yao, Shida walizonazo, najua leo Watanzania wanatuangalia hapa leo, kila mmoja ajiangalie yeye na jirani yake wana maisha gani,” alisema. Alisema kutokana na utajiri ambao Tanzania imebarikiwa ikiwemo kuwa nchi ya pili baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi, Watanzania hawastahili kuishi maisha ya kimasikini.
Awali, wakizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhiwa ripoti za uchunguzi wa biashara ya almasi na tanzanite, wenyeviti wa kamati hizo, Mussa Zungu na Dotto Biteko walibainisha namna kamati zao zilivyoibua madudu ikiwemo kuwepo kwa mikataba mibovu, usimamizi mbovu wa rasilimali hizo za madini namna madini hayo yanavyoibiwa.
Kwa upande wake, Zungu alisema kamati yake ilibaini udanganyifu mwingi ulioitia hasara serikali ikiwemo uwepo wa mitambo ya zamani huku taarifa zikionesha ni mitambo mipya pamoja na kuchenjuliwa kwa makinikia ya almasi yaliyochimbwa miaka 40 iliyopita huku taarifa zikionesha yamechimbwa hivi karibuni. “Tumegundua Stamico iliufanya mgodi wa almasi kama shamba la bibi, yapo madeni ambayo mgodi huu unadaiwa lakini nina uhakika yakihakikiwa yatakuwa si ya kweli, mfano kwa sasa mgodi unadaiwa Dola za Marekani milioni 238, lakini deni hili likihakikiwa haliwezi kufikia dola za Marekani milioni 15,” alifafanua.
Naye Biteko pamoja na kuzungumzia namna serikali ilivyoingia mikataba mibovu kwenye biashara ya tanzanite, pia alieleza jinsi kamati hiyo ilivyobaini kuwepo kwa watu waliokabidhiwa dhamana ya usimamizi wa madini walivyoshindwa kuyasimamia. Alisema katika kamati yake walikuwa na hadidu za rejea tano na walihoji mashahidi 159, walipitia na kuchambua nyaraka 150 za umma na binafsi na kubaini kuwa mkataba uliopo wa tanzanite na Stamico hauna tija kwa taifa. “Mfumo wa usimamizi uliopo ni dhaifu, kwani tanzanite yote iliyochimbwa nchini mapato yaliyopatikana kwa Tanzania ni asilimia 12 tu, wakati madini haya yanayopatikana nchini pekee, yanatoa ajira zaidi ya 500,000 India,” alisema
Magufuli 'Tulitumia Ukachero Kupata Taarifa za Acacia'
6
September 08, 2017
Tags
Inasikitisha na Inauma.....
ReplyDeleteHalafu wanasimama wanaojiita Wasiasa kutetea wizi...!!!
Hapo kweli kuna Uzalendo?
Inasikitisha na Inauma.....
ReplyDeleteHalafu wanasimama wanaojiita Wanasiasa kutetea wizi...!!!
Hapo kweli kuna Uzalendo?
Hivyo kina Kahama na Mmapachu wana sura kati nchi hii...!!!
Ubinafsi na Tamaa Ummetawala....
JPJM Endelea na Kazi na Unataifisha kila kilichopo cha hawa Wahujumu Uchumi
hata kutaka kumuua Lisu nae ulitumia ukachero wa Ruanda.
ReplyDeleteNa bado.........mpaka kieleweke
Deletekitaeleweka siku utayokuwa kaburini.
ReplyDeleteMakachero ni viongozi wetu eote wakuu ambao ambao waliisaini mikatsba hii mibovu na ndio wanasiasa na vigogo wa ngazi za juu wa nchi hii ambao wamepewa kinga na hawa ndio nfugu Lisu amepiga kele na wapinzani bungeni miaka nenda rudi.walikabidhiwa madaraka kulinda mali za nchi hii kwa niaba ya watanzania.ni kati ya vigogo hawa walioisaini hii mikataba ya almasi na dhahabu.wote mnawajua, na haya yote ni mwanadheria huyu Lisu kayapigania wazi na hadharani bila woga.badala ya kuusema ukweli wa mambo ulivyo bado tunamzungumzia mjeruhi ambaye ilikuwa afanyiwe assanation tunamtuhumu. Mungu wa nazareti mbona tunageuza ukweli wa mambo ulivyo na kuwatuhumu wasio na hatia.wenye hatia ambao ndo chanzo cha haya matatizo yote, na wote wadomi mnaojua sheria na kufuatilia mambo haya mnawajua ni akina nani waliosaini mikataba hii, na ni akina nani viongozi walioshindwa kudimamia hizi kazi na wapo huru wamekaa kimya. Ndugu Bashe juzi kasema wazi na kwa hadira bungeni, toeni kinga na mlete katiba mpya. Itaruhusu hawa viongozi wote kuchukuliwa hatua kali. Na ingawa kuna kamata ya skina dingadinga, hakuna kinachoendelea. Upinzani vijana wamepiga kelele sana mpaka wakataja majona na wakaliambia Taifa, kama sheria hazitendi kazi watawakamata wahusika. Tukaona juzi watu wansjiuzuru. Imrchukua upinzani na kulalamika kwa muda mwingi sana kulitimiza hili. Sifa anapewa spika wa bunge. Ns snaambiwa na kipewa amri awafukuze nje. Kwa watu wanaoyafuatilia haya mambo kwa ukaribu sana inachanganya vichwa. Ingawa napongeza kusimama kwa mara ya kwanza kwa raisi kufuatilia na kuanza kutenda kazi, bila upinzani ambao hata hawapewi kauli inayostahili hata siku moja ndicho kinachopasua nchi. Hatupo pamoja. Ccm ni ccm, na vyama vingine vimepews jina baya upinzani na wamefanya kazi kubwa sana kwa tsifa hili kwa shida sana kuwekwa ndani, kuvamiwa, mabomu, wengine wamepotea, na Lisu sasa kupigwa bunduki mchana kweupe.Badala ya kuungana kitsifa, hakuna kiongozi hata mmoja anayefanya hili.na huu ni mpasuko wa nchi na chanzo cha uhasama.watanzania tumekuwa kama watoto, hatutski kuuunaa ukwrli, na tunakubali diasa zitugawe, zituuwe, na kuficha ukweli wa mambo, wsoga, kwa kutunza vyeo na vimishahara. Uongo huu unaanza kudhihirika sasa na kuleta uhassma mkubwa na kuleta vita kati ya wananchi kupitia itikadi zetu na chama gani kimeshika dola. Je hatuwajui watu waliosaini mikatsba, na wanazidi kuisaini . Mnataka kusema mnaturufishia hadhi ya nchi bila kuwawajibidha wshudika wakuu.huwejzi kujenga nyumba na kuezeka bati zinazongaa ukijua msingi mzima ni mbovu. Afadhali kuvunja nyumba nzima ianguke kuliko kungojea nyumba ianguke na kuua wstu walioko ndani. Mfumo mzima ufumuliwe kwanza. Mspapa wachukuliwe hatua kwanza, na ukisafisha na kufagia ndipo taifa litakuwa safi bila harufu. Kwa hapa tulipofikia, di pa kumpigia makofi mtu mmoja. Bali kuona ukwrli halidia na kuungana bila kujali itikadi kama mlivyoungana kumsaidia Lisu kopesa bungeni, bunge lianze kutenda haki ya usawa na kutetea maslahi ya wananchi kihalidia na di kwa kutoa adhabu zisizo za msingi.mkimnyamazisha mwenye hoja mara kumi mnajenga uadui na chuki. Na hili limekuwa tatizo bungeni. Kuna wabunge hoja zao hazina mantiki, ni krlele, cheko, zisizostahili bungeni. Wengi wabunge hawana uwezo kwa mambo mengi sana, sababu ya kisomo, kazi yso kelele hata pasipostahili na kwa sababu ya ueingi wao ndo dheria hafifu zinapitishwa na Taifa linaumia. Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala ni mizoga mitupu. Na kupoteza pesa za walipa kodi. Tuanze utaifa kwanza, kabla ya vyama. Hsya yote ni matatizo makubwa sana yanayochangia misukosuko nchini. Tuombe utashi ili tujue tunschokizungumza ni nini, na athari zake ni xipi. Tusikurupuke, tutsfakari na kufikiri kabla ya kusema neno, tutumie vyeo vyetu kwa unadhifu ni dhamana ya nchi. Tutumie busara na uadilifu. Tujue tunafanys kazi ya nchi si ya nyumba binafsi na kuna mamilioni ya watu kwa kila tunachokifanya kinawathiri.
ReplyDelete