Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.
"Uchaguzi haukuwa na uwazi na hatukuwa na lingine ila kuufuta," jaji alisema.
Jaji Mwilu amesema tume ya IEBC ilitegemea ripoti za waangalizi wa uchaguzi kuamua kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Waangalizi walikosolewa vikali wakati uchaguzi ulifutwa kwa kuharakisha kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wenye uwazi.
Kwa upande wake jaji mkuu nchini Kenya David Maraga, amesema kuwa upinzani hakubaini madai yao kuwa kampeni za rais zilitumia fedha za umma kugharamia kampeni zao.
Jaji Maraga amesema kuwa sampuli kadha za fomu zilionyesha kuwa hazikuwa na mihuri rasmi, zingine hazikwa na sahihi na namba za usajili wala alama rasmi.
Amesema kuwa uchaguzi haukufutwa tu kwa sababu ulikuwa na hitilafu, lakini kile amekuwa akikichunguza ni ikiwa hitalafu hizo zilishawishi matokeo.