Man U, PSG, Barcelona na Chelsea Zilivyoua Ligi ya Mabingwa Ulaya....


MAN U, PSG, BARCELONA NA CHELSEA ZAUA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MANCHESTER United imerejea kwa nguvu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Basel, kama ilivyo kwa wababe wa Hispania, Barcelona waliopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus. Msimu wa 2017/18 wa michuano hiyo hatua ya makundi ulifunguliwa usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na mechi nyingi kwenye viwanja tofauti huu vigogo wengi wakiibuka na ushindi.


MANCHESTER UNITED 3- 0 BASEL
Ikicheza kwenye uwanja wake wa Old Traff ord, United ilipata ushindi huo muhimu katika Kundi A, mpira ukiwekwa wavuni na Marouane Fellaini dakika ya 35 na Romelu Lukaku dakika ya 53, mabao yote yakifungwa kwa kichwa huku Marcus Rashford akitokea benchi na kuifungia timu yake bao la tatu. Katika mchezo huo, kiungo wa United, Paul Pogba aliyekuwa nahodha wa kikosi chake aliumia dakika ya 19 na kutolewa kisha nafasi yake ikachukuliwa na Fellain. Mchezo mwingine wa kundi hilo Benfi ca imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa CSKA Moscow.

CELTIC 0-5 PARIS SAINT GERMAIN
Licha ya kuwa ugenini, PSG ilifanya kweli kwa ushindi huo mnono ikiongozwa na Neymar aliyefunga dakika ya 19, Kylian  Mbappe (34) na Edinson Cavani (40). Mikael alijifunga katika dakika ya 83, huku Cavani akirudi tena kambani na kuifungia timu yake dakika ya 85. Mchezo mwingine wa kundi hilo la B, Bayern Munich ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Anderlecht.

BARCELONA 3-0 JUVENTUS
Ikiwa Uwanja wa Camp Nou, Barcelona ilianza vizuri michuano hiyo kwa kuwachapa vigogo wa Italia, Juventus wafungaji wakiwa ni Lionel Messi (45, 69) na Ivan Rakitic (56) katika mchezo wa Kundi D. Aidha Olympiacos ilipata kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Sporting CP katika kundi hilo.

CHELSEA 6-0 QARABAG FK
Matajiri wa London, Chelsea walipata ushindi huu mnono katika Kundi C wafungaji wakiwa ni Pedro Rodriguez (16), Davide Zappacosta (30), Cesar Azpilicueta (55), Tiemoue Bakayoko (71), Michy Batshuayi (72 na 82), Kipute kingine cha kundi hilo Roma na Atletico Madrid zilitoka 0-0. Mechi nyingine kali za michuano hiyo zinatarajiwa kuendelea leo lakini mechi kubwa ni Liverpool na Sevilla, Spurs vs Dortmund, huku Madrid akicheza na Apoel.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad