Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameleeza kuwa kazi ya upinzani ni ngumu sana.
Mbowe amesema kuwa licha ya vitisho na kila aina ya hujuma wanazofanyiwa kamwe hawawezi kurejea nyuma.
Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.
Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.
Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatenegeneza hasira kubwa ndani ya jamii.
Mbunge Tundu Lissu yupo mjini Nairobi Kenya kwenye matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.