Akijibu hoja hiyo Bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani amesema serikali haina ushahidi na suala hilo huku akidai Umoja na Mataifa wa Mawasiliano Duniani umeweka viwango maalum kwenye ‘head phone’ambacho hakina madhara kwa watumiaji.
“Napenda kujibu swali la Mh Mama Salma Rashid Kikwete mbunge wa kuteuliwa, mama yangu kama ifuatavyo, Mh Spika kitaalam hakuna taarifa za kitabibu kuhusu madhara ya matumizi zaidi ya mara kwa mara ya ‘head phone’ kwa muda mrefu aidha vifaa vyote vya mawasiliano zikiwemo ‘headphone’ huwekewa viwango na Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano Duniani kwaajili ya matumizi salama. Hivyo hakuna madhara ya utumiaji wa vifaa hivyo kwa kuwa vimethibitishwa na kimataifa na kwa hapa nchini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakishirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wana juhumu la kuhakiki viwango vya vifaa vya mawasiliano Tanzania kabla havijaanza kutumika,” alisema Ngongani.
Aliongeza, “Mh Naibu Spika kwa kuwa mimi sio daktari nakubaliana na Mh Mama Salma Kikwete ampeleke mtu ambaye anadai ameathirika na matumizi ya ‘headphone’ kwenye watu wenye dhamana afya ili wakamchunguze na taarifa ya kitatibu ambayo itatoka tutachukua hatua,”
Pia waziri huyo amewataka maredeva ambao wanatumia ‘headphone’ wakati wanaendesha kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
“Naomba nichukue fursa hii kuwahasa madereva ambao wanaendesha vyombo vya moto kutosikiliza simu na ‘headphone’ wakiwa katika mwendo, kama ni lazima kusikiliza simu asimamishe chombo cha moto halafu ndipo asikilize simu, kusikiliza simu huku unaendesha ni kuhatarisha maisha yako pamoja na abiria uliowachukua,” alisema Ngonyani.