Mavunde: Serikali Kuimarisha Sheria Mifuko Ya Jamii



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Antony Mavunde
Serikali imepanga kuwasilisha Bungeni mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii yatakayoanzisha Fao la Upotevu wa Ajira kwa wafanyakazi watakaokuwa wanapoteza ajira kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kazi.

Akizungumza katika kikao cha Tano cha Bunge la 11, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Antony Mavunde amesema Serikali inatambua changamoto ya wingi wa mifuko inayoikabili Sekta ya Hifadhi ya Jamii hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo mwaka 2015 Serikali ilifanya tathamini ya mifuko yote ya Pensheni kwa lengo la kuangalia uwezekano na namna bora ya
kuiunganisha.

“Matokeo ya tathimini iliyofanyika mwaka 2015 yalionesha kuwa inawezekana kuunganisha mifuko hiyo na kubaki na michache kwa kuzingatia hali halisi ya mahitaji”. Alisema Mavunde.
Aidha, Mhe. Mavunde aliongeza kuwa Serikali imeandaa mapendekezo ya kuunganisha
Mifuko mitano inayotoa mafao ya pensheni na kubaki na michache iliyo imara.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa mwaka 1952 fao la kujitoa sio miongoni mwa mafao yalioainishwa katika mkataba huo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad