Mbowe Atoa Sababu Kwa Nini Hawajafungua Kesi Yoyote Dhidi ya Shambulio la Tundu Lissu

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na shambulio Tundu Lissu  ambapo amesema ni kutokana na kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.

Mh. Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.

"Kwa nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.

"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza

Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya kumficha.

"Wiki iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.

Ameongeza pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad