Mbunge Hassan Turky wa CCM Akanusha Taarifa iliyotolewa na Ndugai Kwamba Alilipia Ndege iliyompekea Lissu

Mbunge wa Mpendae, Salim Hassan Abdullah Turky (CCM), amekanusha taarifa iliyotolewa na Spika wa bunge Job Ndugai kwamba alilipa gharama za ndege iliyimpeleka Lissu Nairobi.
Asema Chadema ndiyo waliolipa gharama za ndege hiyo kwenda Nairobi, na yeye alichofanya ni kuwadhamini tu kwa kuwa Chadema hawakuwa na fedha taslimu za kulipia kwa wakati huo.
__
"Hapana sikulipa cash, na bahati mbaya siku ile isingeweza kuruka kama zisingepatikana dola 9,200 kwa maana lazima ulipe ndio ndege iruke. Na hapa Dodoma hakuna mbunge aliyekuwa na hata dola 1,000 hivyo hali ilikuwa ngumu kidogo".
___
Alisema Turky na kuongeza "Kwahiyo Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” amesema.
Mapema leo bungeni, Spika Ndugai alisema ndege iliyompeleka Lissu Nairobi ilikodiwa kwa Dola za Marekani 9,200 na Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah (Turky). .
.
TOA MAONI YAKO HAPA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad