Msukuma ametaka kufanyike uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vifo vya mara kwa mara vinavyotokea ndani ya Mgodi huo akisema kwamba hiyo sio mara ya kwanza kuokotwa maiti ndani ya GGM.
”Kumekuwa na matatizo yanayotokea kwenye mgodi mkubwa wa GGM. Niliwahi kuzungumza Bungeni kwamba kuna watu wanauawa katika mazingira ya kutatanisha lakini Jeshi la Polisi na Serikali ya Mkoa wa Geita haichukui hatua.
“Hali iliyotokea sasa, tarehe 18 imeokotwa maiti ndani ya Mgodi wakapewa watu kwenda kuzika lakini tarehe 23 mtu mwingine amefariki pale na amefariki katika mazingira ambayo wao walidai alitumbukia kwenye shimo – aliteleza kutoka juu.
“Tulipopata ile taarifa ilionesha ana majeraha kichwani ambayo hayalingani na maelezo kwamba ameporomoka kutoka juu.” – Mbunge Msukuma.VIDEO: