MBUNGE Sugu Aitaka FBI ifanye Uchunguzi wa Kupigwa Risasi Tundu Lissu

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema anaunga mkono hoja ya viongozi wengine wa CHADEMA kutaka serikali iruhusu vyombo binafsi vya usalama kuchunguza tukio la Tundu Lissu la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Sugu ameandika ujumbe akisema kwamba serikali iruhusu uchunguzi kutoka vyombo binafsi vya kimataifa, ili kuwatambua na kuthibitisha waliompiga risasi Tundu Lissu.

"Nami naunga mkono kuitaka serikali iruhusu uchunguzi wa kimataifa kutoka vyombo kama FBI au 'Scotland Yard' ili kuwatambua na kuwathibitisha waliohusika na kitendo hiki ili wawajibishwe kwa hili jaribio la mauaji lisilo na maana, na hao wasiojulikana sasa wajulikane", ameandika Sugu.

Pia kwenye ujumbe huo Sugu ameweka wazi kuwa alitakiwa kusafiri kwenda nchini China kikazi lakini amelazimika kusitisha safari hiyo kwa sababu ya matatizo ya Tundu Lissu.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona Congress alipopigwa risasi USA hawakutaka Scotland Yard Kunchunguza. Jirani kenya Scotland mbona hawakutoa report ya kifo cha Ouko mpaka. Chadema acheni kutukana police.

    ReplyDelete
  2. Eti FBI, Kibiti wameuawa ndugu zetu wengi hamkuona shida.Acheni uzandiki.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad