Mbunge wa Rombo Asimulia Jinsi Tundu Lissu Alivyopigwa Risasi

Mbunge wa Rombo, Joseph  Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na  gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.                    

Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.                      

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema                    

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi  na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani mbona hizi habari zinatatanisha!

    "Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi ", Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma."

    " Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata "

    Chadema ni Balaa....!!! inafikia hadi ya kutaka kumpa kilema mwanachama mwenzao .
    Kisa.... Anampiku Mwenyekiti wake...
    Mtajieleza toka HAI mpaka Nyiramba.
    Mlijaribu kwa Maskini Jito akaenda kkukiki huko akti. Sasa huyu bado hajaanzisha chama kipya
    mnataka funga kazi. Haya Dlama ndiyo inaanza.
    Kwani mtigwa amesema nini huko Kihesa??
    Hisia zipo na Dalili ni Dhahiri.
    Cdedma mtatueleza!!!!! na Ben sanane pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad