Mchugaji Peter Msigwa Amfungukia Kamanda Sirro 'Ulitaka Lissu Atoe Taarifa Gani zaidi Polisi? "

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Mbunge Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari ambalo lilikuwa likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa risasi.

"Kamanda Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi wengine ni wanasiasa, hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha yetu kubwa ni kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja inapaswa kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana na vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na mikoa" aliandika Mchungaji Msigwa

Aidha Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa ajili ya kutetea haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema alichofanyiwa Tundu Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.

"Mungu anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi yanitoka kuona rafiki yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea  haki na demokrasia ya taifa letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele, sitanyamaza, tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika Msigwa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msigwa, Umejaribu viongozi wa dini na Waunini wao.
    Sasa Unazungumzia Demoglasi na Haki.
    Unajaribu kuingiza Tuhuma na Lawama ambazo chanzo chake hakieleweki.
    sasa chagua mada na Ujumbe unaotaka kutufikishia.
    Usipoteze mwelekeo na Majira.

    Na kama huna la maana . unaweza kutuelezea kinachoendelea hapo ndani ya chama kutafuta Kiti na Kiki.
    Kama kina Samora na Nkomo na canan Banana/ Eduard de santos /agustine Neto.
    Hao wote wameshapata Uhuru. na ndiyo waliokuwa wa Mwisho mwisho Barani kwetu na Harakati hakuna tena na Hatuzifikirii.
    Usipotoshe Umma we na wenzako wote wenye mwelekeo kama wako. Tanzania ni Huru to zama zile.
    Na sasa Mh. Raisi na sisi tuko katika Vita vya Uchumi na Rasili mali zetu.
    Unataka unaunga mkono hutaki Pumzika na ikiwezekana Unakwenda kulima shamba.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad