Hilo limethibitishwa leo na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma kwenye ukumbi wa Mahakama ya rufaa jijini Dar es salaam.
Jaji Ibrahimu amesema Makamu wa Rais atafungua mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 354 kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola.
Jaji Mkuu amesema katika mkutano huo Tanzania itawakilishwa na wajumbe 50 ambao ni Majaji na mawakili kutoka Tanzania bara na visiwani.
Ujumbe mwingine mzito wa watu 13 ambao ni Marais na Majaji kutoka Austaria, Zambia, Afrika Mashariki na Pakistani utakuwepo kwenye mkutano huo.
Aidha Jaji amebainisha kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein atafunga mkutano huo mnamo Septemba 28 mwaka huu.