Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Mabeyo Aguswa na Tukio la Tundu Lissu...Afunguka Makubwa

Mkuu wa majeshi nchini, Venance Mabeyo amewataka wananchi kutulia kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikipapambana na matukio ya kihalifu wakati wote, akitolea mfano matukio yaliyotokea Kibiti lakini ameshangazwa na mshtuko uliotokea sasa, Mabeyo amesema asingependa kuingia huko lakini vyombo vya ulinzi na usalama vinapambana na matukio kadri yanavyojitokeza na anaamini hali itakuwa shwari.

Jenerali Mabeyo amesema kwa sasa vyombo vya usalama vinashughulika na hoja ya msingi ni kutaka kujiridhisha silaha zinapotoka na watu ni wa aina gani hivyo watu waviache vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake na kuacha kutoa majibu haraka. Ameendelea kwa kusema tukio linapotokea lazima liangaliwe limetokeaje, chanzo nini na dhamira yake.

Swala la pili aliloongelea Jenerali Mabeyo ni uzoefu walionao, vijana wanaofanya uhalifu hawajapitia Jeshi la Kujenga Taifa hivyo wana imani vijana wao wote wanaopitia JKT wanakuwa na nidhamu. VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad