Msajiri wa Hazina: Taasisi na Mashirika 71 Hali Tete


Msajiri wa Hazina: Taasisi na Mashirika 71 Hali Tete
Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano amesema taasisi na mashirika 71 yaliyosaini mkataba wa utendaji kazi mwaka 2014/15 hayakufikia malengo.

Akizungumza leo Septemba 5 wakati wa utiaji saini mkataba wa taasisi na mashirika ya umma 30, Mashindano amesema baadhi zilishindwa kufikia malengo kutokana na mipango yao kutoendana na bajeti.

Amesema baadhi ya mashirika ya umma yameshindwa kukusanya mapato kulingana na mikataba waliyoingia.

Mashindano amesema baadhi ya mashirika ya umma yameshindwa kufikia malengo katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kuhusu mashirika yanayosaini mikataba leo, ametoa wito kwao kusimamia changamoto ambazo zimewafanya wenzao kushindwa kufikia malengo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda ametoa wito kwa viongozi wenzake wa mashirika ya umma na taasisi binafsi kuhakikisha wanamsaidia Rais John Magufuli kusimamia taasisi wanazoongoza ili ziweze kutoa mchango unaostahili kwa Taifa.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad