Msigwa: Tuko Wabung Wanne CHADEMA Tunaowindwa

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa amefunguka na kutaja majina ya wabunge wengine wa nne ndani ya CHADEMA ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana ili kushambuliwa kama alivyoshambuliwa Mbunge Tundu Lissu.

Msigwa amesema hayo leo akiwa jijini Nairobi nchini Kenya ambapo yupo huko kwa ajili ya kumuangalia Mbunge Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi Septemba 7 mwaka huu mjini Dodoma

 Msigwa ametumia nafasi hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kuwa hata wao wanatafutwa na watu wasiojulikana ili kupigwa risasi.

"Usalama wetu upo mashakani niwaambie usalama wa taifa, nimwabie Mkuu wa Majeshi, nimwabie IGP pamoja na Rais mwenyewe tunawindwa wabunge wengine wanne wa CHADEMA akiwepo Mhe. Freeman Mbowe, mimi vijana wale walinifuata wiki mbili zilizopita Iringa, Mhe Godbless Lema alifuatwa Arusha, Halima Mdee na Mhe. Mbowe tupo kwenye orodha hiyo ya kuuwawa" alisema Mchungaji Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa ameendelea kusema licha ya vitisho hivyo wao wataendelea kuzungumza na kukemea mambo ambayo yapo kinyume na utaratibu na sheria za nchi na kusema hawataogopa.

"kwa hiyo hizo roho zetu tumeziweka mikononi mwenu lakini tunasema kwamba hatutanyamaza tutakosoa, tukakemea, na kupinga uonevu wowote katika nchi yetu, kwa haya mambo hamtatutisha wala kutunyamazisha tunaendelea kusonga mbele" alisema Mchungaji Msigwa.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msigwa...!! wewe kakika waatu na wewe Umo? au unajiingiza ingiza.
    Wewe hata katika hesabu ya kuongeza Idadi haupo.
    Usijidanganye na kutuchanganya.
    Na kwa taarifa yako... Hizi siku ambazo haupo hapa Bungeni.Posho kama tulivyo kwambia Tunakukata.

    ReplyDelete
  2. Hayo mapambio ya CHADEMA, kila jambo litakuuzwa.Lakini mkumbuke hadithi ya kijana na Mbwa Mwitu siku itapokuwa kweli kila mtu atajua ni zile kelele za siku zote ilhali mnaumia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad