Mtatiro: Amri ya kumkamata Zitto yatolewa..Lakini Mbona Hatuoni Bunge Likiwahoji Wakuu wa Taasisi Mbali Mbali Kwa Utendaji Mbovu?

Katibu wa Bunge, mhe. Kashililah ameviagiza vyombo vya dola vimsake kumkamata na kumfikisha mhe. Zitto Kabwe mbele ya kamati ya maadili Dodoma. Mimi najiuliza bado, hivi hii ndiyo kazi kubwa ya bunge kikatiba?

Mbona hatuoni Bunge likimuita na kumuhoji Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu kwa kuchukua Mkopo wa Trilioni 1.2 bila kulihusisha bunge na tena mkopo wenyewe ukiwa ghali na malipo yake ni "damu na jasho" za wanachi?

Mbona hatuoni Bunge likiwahoji wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali kwa uzembe na utendaji mbovu?

Mbona hatuoni Bunge likimhoji RPC wa Dodoma kwa hadi leo kushindwa kuwakamata watu waliompiga risasi Tundulisu mchana kweupe tena kwenye eneo lililokuwa linapaswa kulindwa kwa uhakika?

Yani tunashuhudia bunge ambalo kazi yake kuu ni kupambana na wabunge wake, kuwadhalilisha, kuwaogofya, kuwashughulikia na kuwaumiza. Hili ni Bunge la Tanzania kwa mujibu wa katiba?

By Julius S. Mtatiro
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad