Mwadui Watupia Lawama Nyasi Bandia Wasema Ndo Chanzo Cha Kushindwa Mchezo Wao Dhidi ya Simba

Mwadui Watupia Lawama Nyasi Bandia Wasema Ndo Chanzo Cha Kushindwa Mchezo Wao Dhidi ya Simba
Kiungo wa Mwadui, Awadh Juma amesema nyasi bandia zilikuwa kikwazo kwao jana kwenye mchezo wao dhidi ya Simba na hivyo kusababisha baadhi ya wachezaji kupata majeraha.

Wachezaji watatu wa Mwadui akiwemo Awadh na Radhack Khalfan walishindwa kuendelea na mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na  kupata majeraha.

Awadh "Nilishindwa kuendelea na mchezo kwa sababu niliumia  misuli na hiyo yote kwa kwa sababu ya nyasi bandia. Tangu tumekuja tumefanya mazoezi siku moja tu kwenye uwanja huo  na jambo hilo limetugharimu na kusababisha wachezaji watatu kuumia.

Hata hivyo Awad hakusita kukiri kuwa makosa waliyoyafanya ndio yaliyowapa Simba ushindi kutokana na wapinzani wao kutengeneza nafasi nyingi na kuzitumia.

"Wapinzani wetu walitengeneza nafasi nyingi na kuzitumia lakini sisi  hatukutumia hata nafasi chache tulizopata. Tutayafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo ijayo," alisema Awadh.

Tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara, Mwadui imeshinda mchezo mmoja kati ya mitatu iliyocheza huku ikipoteza michezo mwili dhidi ya Mtibwa Sugar na Simba.

Timu hiyo itakuwa nyumbani mchezo unaofuata itakapoikabili Prisons Jumamosi kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga.

 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad