Liliane Bettencourt, ambaye ni mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L'Oreal, amefariki akiwa na umri wa miaka 94, familia yake imethibitisha.
Kauli ya familia inasema kuwa amefariki ''kwa amani'' nyumbani kwake wakati wa usiku.
Huku thamani ya makadirio ya mali zake mwaka 2017 ikiwa ni dola bilioni 33 ama dola bilioni $40 Bi Bettencourtalikuw andiye mwanamke tajiri zaidi duniani.
Aliondoka kwenye bodi ya kampuni hiyo 2012 na baada ya hapo alionekana mara chake katika umma , lakini alisalia katika habari kwasababu ya kesi yake iliyopata umaarufu iliyofuatia kupatikana kwake na ugonjwa wa ubongo.
Katika kauli yake, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya L'Oreal Jean-Paul Agon amesema: "sote tulimuhusudu sana Liliane Bettencourt ambaye wakati wote alisimamia kampuni ya L'Oreal, na wafanyakazi wake, ambaye pia alijivunia maendelea na mafanikio ya kampuni yake.
" Binafsi alichangia sana katika mafanikio yake kwa miaka mingi sana. Mwanamke bora wa urembo ametuacha na hatutamsahau."
Mrithi huyo wa Kampuni ya L'Oreal aliingia katika mzozo wa umma na binti yake , Francoise Bettencourt-Meyers, mwaka 2007.
Bi Bettencourt-Meyers aliwasilisha kesi yake mahakamani ambapo binti huyo alisema ana wasiwasi kwamba mama yake anatumiwa vibaya wasaidizi wake kikazi kutokana na afya yake ikiendelea kuzorota.
Ilifichuliwa mwaka 2008 kwamba mpigapicha ambaye alikuwa rafiki yake, François-Marie Banier, alizawadiwa zawadi zenye thamani ya mamilioni ya dola -ukiwamo mchoro wa Picasso pamoja na kisiwa cha heka 670 katika visiwa vya Ushelisheli.
Bi Bettencourt-Meyers alisema alichukua hatua za kisheria dhidi ya Bwana Banier baada ya kuambiwa na mfanyakazi wa nyumbani wa mama yake kwamba alikuwa anapanga kumuasili.