Nani Anagharamia Matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe Huko Nairobi?

Nani Anagharamia Matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe huko Nairobi?
Kwanza natanguliza pole na kumtakia mema Kamanda wetu Tundu Lissu. Lakini najaribu kufikiri kwanini Msigwa na Lema bado wako Nairobi?

Kwa gharama za nani? Kama za kwao kwanini wasirudi nyumbani kisha hizo fedha wachangie kwenye matibabu?

Tena lile jopo limeambatana na Wake na wenza wao, WHY?

Yawezekana na wao ni sehemu ya matumizi ya fedha zinazochangwa na Watanzania walalahoi........

Jamani rudini nyumbani tuhamasishe michango maisha ya Nairobi ni ghali sana......

By Kurzweil/JF

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wote tunawachangia na hawalali sehemu ya kitoto hata posho tunawalipa sasa hivi wanataka tuchange 550m hii hatarii .chadema kamfuko ka chama kamepata sababu ya kukatumbua

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli ni upuuzi mtupu licha ya kweli Lisu alihitaji huduma muhimu bora na ya haraka kuokoa uhai wake likini suala lake limegeuzwa mtaji wa kisiasa na Chadema kiasi cha kutia kichefu chefu. kwanza kabisa Lisu angeweza kutibiwa hapa nyumbani na pengine angekuwa na hali bora zaidi hivi sasa kuliko huko aliko. Hawa watu wanajiita wazalendo lakini ni wanafiki wakubwa mara kadhaa tumewasikia jinsi wanavyoipigia debe nchi jirani na kuitangaza licha ya nchi hiyo wanaoisifu kuwa ina mfumo mzuri wa kisiasa lakini nchi hiyo imeoza katika kila corruption. Si nchi ya kuilinganisha hata kidogo na kasi ya Tanzania ya sasa katika kupambana katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na nchi bora kabisa barani Africa. Hawa watu ndio waliokuwa wakitudang'anya yakuwa wakipata serikali watakuwa watu wa kubana matumizi lakini sasa imejidhihirisha kuwa ni wanafiki. Lisu kapigwa na kama kweli kapigwa kwenye harakati za kupigania nchi kama wanavyodai cha kusikitika na kulilia hovyo kitu gani? Kila harakati kwa mzalendo wa kweli zina gharama zake na inapotokezea mwanaharakati wa kweli kufikwa na masahibu kamwe sio mwisho wa harakati na kuanza kampeni ya kuiangamiza nchi kwa fitna za kipumbavu za kuwagawa watanzania. Sadamu Husein alikuwa na uwezo wa kila hali kifedha na kadhalika za kuondoka iraq kabla ya maafa. Nnchi kadhaa zenye nguvu ikiwemo Urusi zilimuomba kumpa hifadhi lakini alikataa nakusema kuwa kadhaliwa Iraq atakufa Iraqi hata kama ndugu zake ndio wanaofanya kampeni ya kumuangamiza. Halikadhalika Muamari Gadaf alibembelezwa vya kutosha na nchi marafiki kumpa hifadhi lakini alikataa nakusema Libya ndipo sehemu sahihi kabisa kwa yeye kufikwa na umauti sio sehemu nyengine licha ya kujua yakwamba ndugu zake wameshanunuliwa na wana haha kuisaka damu yake kwa ghrama yeyote ile na kweli Gadafi alikufa kikatili licha ya mazuri yote aliyowanyia watu wake. Basi kama ni uzalendo wa mtu kwa nchi yake hawa akina sadamu ni wazalendo wa kweli kwa nchi zao wala si wanafiki na cowards kama wanasiasa wetu wanajiita wapambanaji wakati ukweli ni kwamba wapambaji wa unafiki na wasaliti wakubwa kwa nchi yetu. Watanzania wenye akili zao hawana haja ya kuilaumu serikali chama tawala hata kidogo kwani wamekuwa wakiendesha hii nchi kwa amani miaka mingi tu ila utaona vyama vya upizani vimeamua kuendesha siasa zao kwa njia za uhasama na serikali na hapo ndipo tunayaona haya yanayotekea na hao wapinzani wasipobadilika basi watanzania tutashuhudia mengi ya kushangaza kwani serikali iliopo madarakani si ya kuremba kwani lengo ni kuindosha hii nchi hapa ilipo katika hali duni na kuifikisha patamu katika maisha bora zaidi na hii ni vita na si ya mdomo mtupu bali ni ya vitendo hasa na tunamuomba muheshimiwa raisi na serikali yake wazidi kukadha buti watanzania tupo nyuma yenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad