Mh. Ole Nasha ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye ambaye alihoji juu ya vigezo vya kupatikana kwa watendaji wa vyama vya ushirika nchini (TCDC) kupitia mfumo wa ushindani kuliko ilivyo sasa ambapo vigezo vilivyopo havina ushindani.
Naibu huyo amesema kuwa sifa za upatikanaji wa watendaji wa vyama vya ushirika zinajitosheleza ambazo ni kuanzia elimu ya kidato cha Nne na kuendelea hivyo kama kuna uzembe unafanyika ni kukosa uadilifu kwa viongozi hao na sio suala la elimu kama inavyodaiwa.
Mh. Nape amekuwa akilalamikia suala la wananchi wa Lindi na Mtwara kutofaidika na zao la Korosho ilihali ndio zao lao kuu la biashara.