Nape Nnauye: Gari Lililotumika Kumshambulia Lissu Limewahi Kuripotiwa Kuwa Linawafuatilia Baadhi ya Wabunge

Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.

"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.


Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ACHA KUTAFUTA KIKI KUPITIA MATATIZO YA WATU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmh, si kila mahali watu wanahitaji kiki. Hakuna kitu chochote naamini anachokulenga Nape kisiasa wala kibiashara, ila naye anajaribu kupambana na haliyake. Nilimuona Bashe akiongea Bungeni kwa busara na hekima nyingi juu ya hili na bahati spika na wabunge wamemsapoti pia. Hata Lisu alionekana mpuuzi flani hovi wakati anaongea, mwishowe risasi 32 zinaelekezwa kwake. Kwani wewe hukuona Nape alipopewa amri ya kurudi kwenyegari na yule jamaa mrefu asiyejulikana? Tena mbele ya kamera? Wewe uko salama lakini hujui mwingine anapitia yepi? Watanzania wa leo si watu tunaojenga Taifa la leo na karne zijazo, badalayake tunaangalia sisi leo tumepata nini. Tambua ya kwamba hiki unachopata au ninachopata kidogo hakiwezi kuwa sustainable na kikawafaa wajukuu na wajukuu zao. Huwa tunapenda kuwasifia watawala hata kama wanakosea jambo au wanatumia approach zisizo kwa mambo mema. Tambua ukimkosoa unamsaidia zaidi a unajisaidia wewe kuliko unapomsifia tu. Yeye ni mtu kama wewe na mimi na sifanyingi zinaweza kumharibu badala ya kumjenga. Tulimsifu Nyerere kaondoka tunamkosoa, tulimsifu mwinyi badae tunamkosoa, Mkapa nae badae tunakosoa, kikwete hayohayo nae. Sasa tumemuacha mtu miaka kumi halafu tunakosoa akiwa nje hiyo akili jamani. Hebu hata kama hatupendi kuambiwa lakini tutafakari kidogo

      Delete
    2. Lucas, Wewe Una mwelekeo wa Kulenga Watawala... !!!
      Hii inaonesha upeo wako wa Kufikiri na Uamuzi Umesha tolewa na Kichwa Chako.
      Sivyo Mwangu.
      Usijikite Upande wowote .. ikiwa Unataka kupata mwelekeo sahihi.
      Kuna baadhi ya wenzetu huwa wajifanya waflme katika matumizi ya posho tunazopata.
      na Kuna watu wanalala na Njaa hata ndururu wa kwenda Kula au kujitibu hosptali hawana.
      Hivi sasa ndiyo Baba JPM anapigania rasilimali zetu zisiibiwe na kuleta maisha mema kwa Mtanzania. Tumshukuru mungu kumpata na tumpe sapoti yetu.
      NA HAYA MNAYOA ANDIKA NA POSHO KWA SIKU UNAJUA MILIONI NGAPI??

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad